Y-Dash Kujipiga pini mwezi ujao
Kutoka ndani ya kundi la TMK Wanaume Family, ShowBiz ilidondishewa ishu kwamba msanii Yassin Habib ‘Y-Dash’ yupo kwenye mazoezi makali akijiandaa ‘kujipiga pini’ (kufunga ndoa) mapema mwezi ujao.
Kwa mujibu wa meneja wa kundi hilo, Said Fella, Y-Dash atafunga ndoa ya kawaida na mchumba wake wa siku nyingi ambaye jina lake bado ni siri kwa sherehe itakayohudhuriwa na mastaa kadhaa waliyopo kunako game ya Bongo Flava.
Aidha, safu hii ilihabarishwa kwamba, mshikaji wake wa karibu na Y-Dash, Yesaya Ambilikile ‘YP’ aliyefanya vyema kupitia ngoma yenye jina la Dar Mpaka Moro naye pia ameshatangaza kumchukua jumla mzazi mwenzie ili kumaliza ubishi kwa wale mabinti waliokuwa wakimfuatilia kwa karibu zaidi, siku na tarehe ataitaja siku chache zijazo.
Vijana hao wawili kwa pamoja, tayari wameshadondosha albamu yao mtaani ikiwa na jina la ‘Mapengo matatu’ na jumla ya traki kumi zikiwemo Sweet, Usibweteke, Safari ya muziki, Shania, Kawaambie na nyingine kibao.
********************************************************

Mwana FA Kutaja sababu za kutooa hivi sasa
Kijana Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA au Binamu, siku chache zijazo anatarajia kuweka wazi sababu zinazomfanya asifikirie kutafuta mchumba na kufunga naye ndoa kwa wakati huu.
Akipiga stori na ShowBiz, Binamu alisema kwamba sababu zote ameziweka ndani ya wimbo wenye jina la ‘Bado Niponipo’ ambao amemshirikisha Miss Universe 2007, Flaviana Matata.
“Ndani ya kazi hiyo nimeeleza sababu zote zinazowafanya vijana wengi washindwe kuoa hivi sasa nikiwemo mimi, sababau kubwa ikiwa ni mambo ya ajabu yanayofanywa na akina dada wengi ambayo huwakatisha tamaa wanaume wenanaotarajia kuoa.
“Naachia ngoma hiyo kama fundisho kwa vijana hasa wa kike wenye tabia za kuchanganya wanaume wengi kwa tamaa ya kujipatia pesa,” alisema Mwana FA.
Kazi hiyo mpya ya FA imefanyika chini ya mtayarishaji, Harmy B. Vichwa vingine vilivyofanya fujo ndani ya kazi hiyo ni pamoja na Ambwene Yesaya ‘A.Y’, Alan, Jabir, Shehe na mwanadada Anna. Safu hii ilipata fursa ya kuisikiliza ngoma hiyo na kubaini kwamba, msanii huyo anakuja kivingine na huenda ikamsimamisha kwenye chati za juu.
****************************************************
Mbasha Kutambulisha mbele ya Waziri Mkuu
Staa wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha anatarajia kutambulisha albamu yake mpya na ya tatu yenye jina la ‘Furaha yako’ Juni 29, mwaka huu Mkoani Dodoma, Hamida Hassan anashuka nayo.
Ndani ya safu hii Mbasha alisema kwamba, safari hii ameamua kuanzia Dodoma ili mashabiki wake wa mkoani humo waburudike na kuingia katika imani ya wokovu. “Nawaomba wahudhurie kwa wingi katika tamasha kubwa ambalo litafanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri Dodoma,” alisema.
Msanii huyo amesema kuwa, katika tamasha hilo Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Peter Pinda atakuwa mgeni rasmi, pia watakuwepo viongozi wengine wa serikali.
“Pia nitazindua mtandao wangu (website), www.florambasha.com. Baada ya Dodoma tutaelekea katika mikoa mingine kama Mwanza, Musoma, Arusha na kwingine kwa ajili ya kutoa burudani hiyo ya uzinduzi na kuitangaza Injili zaidi,” alisema Mbasha.
Kelly Kuitangaza Bongo mbele zaidi
Staa wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Kelly Rowland aliyokuwa Bongo kwa siku kadhaa huenda akaitangaza vyema Tanzania mbele zaidi (karibu ulimwengu mzima) kufuatia ziara yake nchini ambayo ilikuwa na mafanikio, Christopher Lissa alikuwepo kwenye msafara.
Akiwa katika jiji la Kandoro, staa huyo alikuwa akirekodi matukio mbalimbali katika sehemu alizokuwa anakatiza zikiwemo uswahilini kwaajili ya kuandaa bonge la documentary ambayo itarushwa kupitia kituo maarufu cha luninga, MTV na kwenye tovuti yake.
Miongoni mwa sehemu ambazo zinaonekana kupewa shavu nene katika documentary ya staa huyo ni pamoja na eneo maarufu la Uwanja wa Fisi lililopo Manzese, Dar es Salaam ambapo Kelly alitia maguu na kuchukua picha za kutosha.
Aidha, binti huyo alipata fursa ya kutembelea mgahawa maarufu wa Rose Garden na kurekodi baadhi ya mambo yanayofanyika usiku katika eneo hilo pamoja na kuzungumza na baadhi ya wasichana wanaofanya biashara ya ukahaba maeneo hayo.
Kelly ambaye ni mmoja kati ya mademu watatu waliokuwa wanaunda kundi la Destiny’s Child alioneka kuguswa na hali duni ya maisha ya Wabongo wengi na kuahidi kwamba, kupitia documentary atakayoandaa ataweza kuleta mabadiliko kiaina.
Kelly alidondoka Bongo mwanzoni mwa wiki hii kupitia mfuko wake, Staying Alive Foundation chini ya udhamini wa MTV ambapo alimwaga misaada mbalimbali na kuahidi kuleta neema zaidi.

1 comment:
mbona hatuambiwi kama alipigha sehemu nzuri pia kama mahoterin,mlima knjaro,urduzungwa,usambara,na mbuga kibao,au hata bagamoyo
japo hali mbaya u/fisi panatisha na nchi imeshindwa kudhibiti,lakini si dhani kama italeta picha nzuri mbele ya mataifa hisani
tunasubiri kelly aje ndo tuamke?hata sisi wanahabri baada yakushauri njia ya kurejkebisha naona tunasheherekea kinchotokea mahala kama u/fisi
hatari kwelikweli
Post a Comment