YOU ARE WHAT YOU EAT
KAMA kuna bidhaa muhimu na inayotumika kila siku majumbani mwetu, basi ni chumvi. Ni bidhaa muhimu katika chakula katika kukifanya kiwe na ladha nzuri mdomoni. Pamoja na umuhimu huo, bidhaa hii ispotumiwa ipasavyo, huwa hatari kwa afya ya mlaji.
Utumiaji wa chumvi katika chakula, hutofautiana kati ya mtu na mtu. Kuna watu wanapenda sana chakula chenye chumvi na wengine hawapendi sana. Kimsingi kiwango cha chumvi anachopaswa kula mtu kwa siku ni kidogo, lakini kwa bahati mbaya sana watu wengi wanatumia kiwango kikubwa cha chumvi kuliko kawaida.
Matumizi ya chumvi yana uhusiano mkubwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure, au Hypertension), kuvimba kwa enka (Swollen Ankles) na ugonjwa wa meneria (Meniere’s syndrome).
Matumizi ya chumvi yanaweza kukusababishia, kukuepusha ama kukusaidia kupona haraka magonjwa hayo. Hivyo ni muhimu sana kujua matumizi sahihi ya chumvi ili kujiepusha na uwezekano wa kupatwa na magonjwa tajwa na mengine.
Chumvi, kitaalamu inajulikana kama ‘sodium chloride’. Vitu vyote viwili, sodium na Chloride, ni vitu muhimu katika lishe. Hata hivyo, vitu vilivyomo kwenye chumvi vinapatikana pia katika vyakula vya asili, hivyo kuongeza chumvi kwenye chakula chenye chumvi yake ya asili siyo muhimu na hata usipoweka huna utakachopungukiwa.
Kwa kuwa matatizo mengi ya chumvi hutokana na wingi au uchache wa sodium mwilini, wakati wa kupima tatizo la kiafya alilonalo mtu kutokana na chumvi, huangaliwa kiasi cha sodium alichonacho mwilini.
Chumvi (sodium) hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo ama jasho. Watu wanaofanya mazoezi ya kutoka sana jasho hutoa kiasi kingi cha sodium tofauti na watu wasiofanya mazoezi ya kutoka jasho jingi. Mtu huyu huhitaji kuingiza mwilini kiwango cha kutosha cha chumvi ili kuepuka upungufu, lakini haina maana anatakiwa kuzidisha kiwango kinachokubalika.
Kiwango cha chumvi kinachopendekezwa mtu kutumia kwa siku, ni kati ya miligramu 920 – 2,300, (kiasi cha robo mpaka nusu kijiko kidogo cha chai), lakini utafiti unaonesha kuwa idadi kubwa ya watu, hasa katika nchi zilizoendelea au watu wenye maisha mazuri, wanatumia zaidi ya kiwango hicho kwa zaidi ya nusu na wengine hadi mara tatu ya kiwango cha kawaida. Kijiko kidogo cha chai kina wastani wa gramu 4.
Iwapo mtu unataka kujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine tuliyotaja, ni vizuri sana kufuata kanuni za ulaji sahihi ambao unasisitiza ulaji wa matunda, mboga mboga kwa wingi, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, hasa ya wanyama, pamoja na kula vyakula vyenye kiasi kidogo cha chumvi.
Watu hujikuta wakila kiwango kikubwa cha chumvi kila siku, wakati mwingine bila wao kujijua kutokana na kupenda kula vyakula vya kwenye makopo ama vile vilivyokwisha tengenezwa ambavyo vingi huwa na chumvi nyingi, ambayo huwekwa, pamoja na sababu nyingine, ili kuongeza uhai wa bidhaa hiyo.
Mara nyingine ukienda kununua bidhaa ya chakula ‘super market’, hakikisha unasoma lebo yake upande wa vitu vilivyotumiwa kuandaa bidhaa hiyo (Nutritional Facts au Ingredients). Hakikisha bidhaa hiyo ina kiwango kidogo cha chumvi (low sodium), kwa kawaida kiwango kidogo kinapaswa kuwa si zaidi ya milligram 120 za sodium kwa gramu 100 ya chakula (120 mg/100 g).
Kubadilisha kiwango cha ulaji wa chumvi, kunaweza kusikuepushe moja kwa moja na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, hata kama kulitokana na matumizi mabaya ya chumvi, lakini angalau kutakusaidia sana kufanya hali isiendelee kuwa mbaya. Hivyo kufanya mazoezi na kula chumvi kidogo kunaweza kupunguza pia hata kiwango cha dawa za presha unachotumia.
Kwa mujibu wa utafiti kuhusu matumizi ya chumvi uliofanyika nchini Australia, watu wengi wanaoishi katika nchini zilizoendelea wanatumia kiwango kikubwa cha chumvi kuliko jamii za vijijini ambao hata wanapokuwa na umri mkubwa hawawi na matatizo ya presha kama ilivyo kwa jamii nyingi zilizoendelea ambazo ugonjwa wa presha unaongezeka na umri.
Kwa kumalizia, mkazo unawekwa kwa watu kupenda kula vyakula vyenye virutubisho mwilini na kuongeza matumizi ya madini joto (Iodine) yanayowekwa kwenye chumvi na kupunguza matumizi ya chumvi, kama ilivyo agizo la serikali la kutaka chumvi inayotumika ni ile yenye madini joto, ingawa haijulikani kama unafanyika ufuatiliaji.

No comments:
Post a Comment