Wednesday, July 2, 2008

HAYA NDIYO 'MADUDU' YA KILI AWARDS!

Bushoke aikataa tuzo ya Kili, awarudishia

Na Saleh Ally
Msanii Ruta Bushoke ametangaza kuirudisha tuzo ya muziki ya Kilimanjaro aliyotunukiwa mwishoni mwa wiki.

Bushoke alishinda tuzo ya wimbo bora wa ‘zouk’, kwenye tamasha lililofanyika kwenye Hoteli ya Kempinsky jijini Dar es Salaam.

Bushoke alitwaa tuzo hiyo kupitia wimbo wa ‘Mbali Nami’ lakini amesema wimbo huo si wa kwake na unaitwa ‘Usiende.’

Akizungumza jana na Mwanaspoti Bushoke alisema ameamua kurejesha tuzo hiyo kwa kuwa wimbo pamoja kwamba ameutunga yeye, lakini ni mali ya Juliana Kanyomozi wa Uganda.

“Mimi sielewi hawa mabwana wanafanya kazi vipi, kama ni nyimbo zangu zipo nyingi tu lakini kwa wimbo huo walipaswa kuwasiliana na mimi hata kunieleza nimeteuliwa badala ya kukurupuka na kunipa tuzo ambayo si yangu,” alilalamika.

“Ingekuwa tuzo ya uandishi wa wimbo ingekuwa yangu, lakini tuzo ya wimbo inatakiwa kwenda kwa Juliana kwa Juliana. Kwenye redio nyingi sana wimbo huo upo kwenye ‘tip 10’ na unatangazwa kuwa ni wa Juliana Kanyomozi akiwa ameshirikiana na Bushoke sasa wenyewe lipi hapo ambalo hawakujua,” alihoji msanii huyo.

Meneja wa Bushoke, Athuman Tippo naye alisema wamechukua uamuzi huo wakiamini ni wa busara kwa kuwa isingekuwa vema Bushoke kujivunia kitu ambacho si chake.

“Bushoke ni kati ya wasanii bora na ana uwezo wa kufanya vitu vikubwa hivyo si vema akachukua tuzo ya mtu hata kama amepewa. Ipo siku atafanya hivyo kwa uwezo wake mwenyewe sababu anao,” alisema.

Bushoke, ambaye ni mtoto wa mkongwe katika miondoko ya dansi Maximilian Bushoke sasa anatamba na wimbo wa ‘Dunia Mapito’ ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya albamu yake mpya.

Msimamo huo wa Bushoke umezidi kuonyesha namna utoaji wa tuzo za Kilimanjaro unavyoyumba na kusababisha lawama kwa wasanii mbalimbali.
Nini maoni yako katia tuzo hizi msomaji?

2 comments:

Anonymous said...

kwa kweli hapo Kil Award wameshemsha sana. hiyo tuzo alitakiwa apewe TID. waache ubabazi

Mrisho's Photography said...

Tatizo waendeshaji sio wadau wa muziki, wamekaa kibiashara zaidi na siyo kuendeleza wasanii wa tanzania kama alivyokusudia muasisi wake marehemu Dandu, kila mwaka wadau wanakosoa lakini hawajirekibishi na matokeo yanapangwa mezani tu...laiti kama angefufuka leo na kuona madudu yanayofanywa katika tuzo hizi, angelia sanaa!