Kitu kimoja ambacho kimeipatia sifa familia ya Zorro ni kipaji cha muziki. Wana kipaji cha kuzaliwa ambacho kimeanzia kwa baba hadi kwa watoto na muziki wanaoimba si wa 'kitoto'. Hebu sikiliza nyimbo za Mzee Zahir tangu enzi zile akiwa JKT Mafinga, akiimba wimbo wa kulipongeza jeshi la Wananchi wa Tanzania baada ya kumuondoa Idd Amin wa Uganda.."Tulikuwa tuko halua wazazi wetu...." hadi sasa anapoimba nyimbo za kizazi kipya kama 'Nzela' wa mwanae Banana Zorro. Ukija kwa mwanae ndiyo balaa zaidi, dada yake nae Maunda Zorro naye ni moto wa kuotea mbali, hakika hii ni familia ya kipekee nchini Tanzani katika medani ya muziki!!!
No comments:
Post a Comment