Friday, August 8, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Nelly:Miss globalpublisherstz.com ni matawi ya mbali

Miss globalpublisherstz.com 2008, Nelly Kamwelu amesema kuwa anajisikia faraja kupita kiasi kwa kushinda taji hilo kwa kuwa hadhi yake ni kubwa kama matawi ya mbali kwenye mti mrefu.

Akilonga ‘ki-showbiz’ hivi karibuni, Nelly alisema, kushinda taji la Miss globalpublisherstz.com kumemuongezea mzuka mara mbili zaidi ya ule aliokuwa nao kwa kuwa sasa anajiamini kwamba ana mvuto wa kutosha.

“Ni shindano ambalo lilikuwa huru, kwa sababu upigaji kura ulikuwa wazi, kwahiyo mimi kushinda kumenifanya nijione kuwa nina mvuto wa kutosha,” alisema Nelly na kuongeza: “Naomba na mwaka ujao shindano hili liwepo ili Watanzania nao wawe na nafasi ya kumchagua mrembo wao.”

Miss globalpublisherstz.com, ni taji ambalo liliandaliwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprise Ltd ambayo inachapisha magazeti ya Uwazi, The Bongo Sun, S&C Magazine, Amani, Ijumaa Wikienda, Risasi, Championi na hili la Ijumaa. Waliokuwa wanawania taji hilo ni washiriki wote wa Vodacom Miss Tanzania 2008.

Lengo la shindano hilo ni Global kuiunga mkono Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi, Vodacom ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa Miss Tanzania kwa jitihada zake za kuiendeleza fani ya urembo nchini.

Shindano hilo, lilikuwa linaendeshwa kupitia tovuti ya global, www.globalpublisherstz.com ambapo majina na picha za washiriki wote wa Vodacom Miss Tanzania 2008, viliwekwa mtandaoni na kuruhusu wasomaji kumchagua mrembo wao.

www.globalpublisherstz.com ni mtandao unaotembelewa kwa wastani na watu 20,000 kwa siku na tangu ulipozinduliwa karibu mwaka mmoja uliopita, umekwishatembelewa na wasomaji wanaokaribia milioni tatu.

Faida za mtandao huo kwa wale wanaoutembelea mara kwa mara ni kupata habari mpya na matukio mapya katika picha ndani ya muda mfupi, kusoma hadithi za mwandishi mahiri nchini, Eric Shigongo, kujionea vivutio vya kitalii Tanzania na mambo mengine mengi.
***************************************************
ZaiN kumdondosha Shaggy leo
Kampuni ya simu za mkononi, Zain ambayo awali ilifahamika kama Celtel, kwa kushirikiana na Prime Time Promotion, leo Ijumaa itamdondosha mkali wa Dancehall, Shaggy kutoka nchini Jamaika ambaye atapiga bonge la shoo ndani ya Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.

Zain ambayo pia imempata mtoto mwenye jina hilo ambaye alizaliwa katika Hospitali ya Mwananyamala usiku wa uzinduzi wa kubadilisha jina la Celtel, imekuja upya katika Tasnia ya Burudani na kwa kuanza itasababisha shangwe za mkali huyo kutoka Jamaika.

Mtoto huyo, Zain Ally Sekondi ambaye alikuwa wa kwanza kuzaliwa hospitalini hapo muda mfupi baada ya saa 6.00 usiku wa Ijumaa Agosti Mosi, mwaka huu alipewa zawadi mbalimbali na Kampuni ya Zain, huku ikiahidi kufuatilia ukuaji wake na kuangalia maendeleo yake kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Prime Time Promotion, Godfrey Kusaga alisema kwamba, wameamua kumleta tena Shaggy ili kuwaridhisha mashabiki wengi ambao hawakupata nafasi ya kumcheki alipokuwa anaagusha ngoma zake pale Diamond Jubilee mwaka 2006.

Akiwa na wasanii wenzie kibao kama Robert Browne, Bruce Brewster, Fabian Smith na wengine, Shaggy ambaye hivi sasa anakimbiza na mawe kama ‘Church Heathen’ na ‘Bonafide Girl’, siku hiyo atatambulisha kazi mpya kibao ambazo wewe shabiki wake haujapata kuzisikia.

“Kutoka Bongo, wasanii kama Prof. Jay, Mwana FA, A.Y, Ray C, Matonya, Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi watapanda jukwaa moja na Shaggy, huku Obsession kutoka Uganda wakiongeza nguvu katika shoo hiyo,” alisema Kusaga.
***************************************

Langa bai bai
Kutoka ndani ya mpambano wa kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop, ShowBiz imepewa ruksa ya kutamka kwamba, leo ni zamu ya Langa kuliaga shindano baada ya kupata kura chache zinazoendelea kupigwa na wasomaji wetu.

Kwa mujibu wa mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso, Langa anakuwa mshiriki wa nne kutoka, akiwafuatia Kala Jeremiah, Black Rhino na Rado aliyetolewa wiki iliyopita na kulifanya shindano libaki na wakali wa Hip Hop sita ambao ni Joh Makini, Lord Eyes, Chid Benz, Prefesa Jay, Fid Q na Kalapina.

“Siyo kwamba mshiriki anayetolewa hayuko safi katika game ya muziki wa Hip Hop, bali tunaheshimu kura za wasomaji ambao ndiyo majaji wa mpambano huu. Tunawaomba wasomaji waendelee kupiga kura zaidi wakimtaja mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa Ijumaa King Of Hip Hop.

“Utaratibu wa kupiga kura ni ule ule, unaandika neno HP, unaacha nafasi, unaandika jina la msanii kisha unatuma kwenda namba 15551. Wasomaji pia mmeandaliwa zawadi zenu, hasa kwa wale watakaopiga kura nyingi zaidi,” alisema Mateso.
(credits: MC GEORGE)

No comments: