Mkurugenzi Mkazi wa Constella Futures, Bi. Halima Shariff (kulia) akisisitiza jambo katika semina ya kuhamasisha kuwepo kwa sera ya ukimwi sehemu ya kazi. Semina hiyo imefanyika leo Millenium Towers Hotel. Kushoto ni Bw. Paul Luchemba wa Contella Futures. Bw. Lucas Mnyaku, muwezeshaji wa sera ya ukimwi kazini, akitoa mada kwenye semina ya mameneja wa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji na umuhimu wa sera hiyo sehemu za kazi, leo Mellenium Towers, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Constella Futures, Halima Shariff (kushoto) akiongea na vyombo vya habari wakati wa semina hiyo.
Shirika la Kimataifa la Constella Futures chini ya udhamini wa USAID -HEALTH INITIATIVE POLICY leo imefanya semina na mameneja na wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini kuhusu utekelezaji wa sera ya ukimwi katika sehemu zao za kazi. Kila media house nchini imetakiwa kuwa na sera hiyo. Pichani ni baadhi ya wanasemina hao kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
No comments:
Post a Comment