Monday, August 18, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Nancy Sumary
Nakaaja Sumary

Fideline Iranga

Full kujiachia
Baada ya wasomaji wengi wa Ijumaa Wikienda kuvutiwa na K-Lyin wiki iliyopita ambaye aliwafunika Ray C na Besta, safu yako ‘Full Kujiachia’ hii hapa tena hewani ikiwa na mabinti watatu kama unavyowacheki pichani.

Unachotakiwa kufanya wewe msomaji ni kututumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kutuambia kwamba, kama utapata nafasi ya kujiachia faragha na mmoja kati ya warembo hawa, Fideline Iranga, Nakaaya na Nancy Sumari utamchagua nani?

Anwani zetu ni zilezile, e-mail:wikienda@globalpublisherstz.com, simu 0713-403-202 na 0715-110 173. Kumbukeni kwamba, wiki ijayo tutachapisha maoni yenu bila kuwabania kwasababu bila nyinyi safu hii haijasimama bado.
*********************************************
Sugu kudondoka Bongo na wataalamu wa muziki kutoka Ulaya
Mwana Hip Hop mkongwe, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu aliyetimkia Marekani anatarajia kuanguka nchini hivi karibuni akiwa na wataalamu wa muziki kutoka kunako nchi kadhaa za Ulaya ambao watatoa elimu inayohusu wasanii kuuza kazi zao kupitia mitandao.

Akisema na Abby Cool & MC George Over The Weekend kwa njia ya mtandao wa itaneti, Sugu alitamka kwamba, pamoja na muziki wa Bongo Flava kusambaa karibu dunia nzima hivi sasa, bado wasanii wanashindwa kufanya biashara kupitia mitandao kama ilivyo kwa wanamuziki wa Ulaya ambao wamekuwa wakijikamulia mkwanja wa kutosha kupitia njia hiyo.

“Kutokana na wasanii wengi wa Bongo kutokuwa na uelewa kuhusu mchongo huo, ujio wangu na wataalamu hao unaweza kuleta mapinduzi mengine katika sanaa yetu ikiwemo kubadilisha maisha ya wengi. Tukifika Bongo tunatarajia kutoa darasa kwa wasanii kwa muda wa wiki mbili. Mimi kama mwenyeji wao nitatangulia kuja wiki moja kabla kwa ajili ya kuwaandalia sehemu ya kufikia, kisha wageni hao zaidi ya thelathini kutoka Marekani, Uingereza, Jamaika na kwingineko duniani watafuatia,” alisema Sugu. Wasanii wa Bongo Flava, mpo hapo?

************************************************

Complex kukumbukwa wiki hii
Msanii aliyewahi kujitoa kwenye game ya muziki wa Hip Hop Bongo, Simon Sayi ‘Complex’ (pichani juu) ambaye alifariki katika ajali ya gari Agosti 21, mwaka juzi atakumbukwa wiki hii kupitia tamasha lenye jina la Remember Agost’ litakalofanyika Ijumaa ya wiki hii ndani ya Ukumbi wa Afri Centre uliyopo Ilala, Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, George Alphonce alisema kwamba, wasanii kibao wanaofanya sanaa ya Bongo Flava watakuwepo siku hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, baadhi yao ni A.Y, Braton wa Backyard Recors, Fid Q, Wanaume Family, Prof, Jay, Mwana FA, Wagosi wa Kaya, Dany Msimamo, Joan, Madee, Gabbo Man na wengine kibao wakiwemo wale waliowahi kufanya kazi na marehemu, ambapo kwa heshima watapata nafasi ya kuongea mawili matatu kuhusu Complex.

“Mbali na kumkumbuka Complex, pia itakuwa ni siku maalum kwa ajili ya kuwakumbuka wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki, ambao kwa namna moja au nyingine walijitoa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia fani zao. Kiingilio katika tamasha hilo ni shilingi 3,000 na sehemu ya mapato itakwenda kumsaidia mtoto wa marehemu Complex,” alisema George.

***********************************************
Mkali mmoja kurudi wiki hii
Black Rhyno
Langa

Rado

Kala Jeremiah
Mshiriki mmoja ambaye ataonekana ni mkali wa michano mbele ya wasomaji na wapenzi wa muziki wa Hip Hop ambaye alitolewa na wasomaji ambao ndiyo majaji ndani ya shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop , wiki hii atarudishwa kuendelea na safari.

Mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso aliwataja wasanii wanne waliyotolewa, ambao wanawania nafasi moja ya kurudi kundini kuwa ni Langa, Kala Jeremiah, Black Rhino na Rado, sababu kubwa ni kuheshimu maoni ya wasomaji na wapenzi wa sanaa hiyo, kwamba mmoja aliyetolewa alistahili kuendelea.

“Tulihesimu maoni yao, tunaomba wasomaji wampingie kura ya kurudi mmoja kati ya hao wanne waliyotolewa, mshindi atatangazwa Ijumaa ya wiki hii kupitia Gazeti la Ijumaa ambalo ndilo huandaa shindano hilo. Zoezi la kupiga kura liko vilevile, unachotakiwa kufanya msomaji ni kuandika neno HP, unaacha nafasi, unaadika jina la mshiriki ambaye unadhani anastahili kuendelea na safari ya mpambano huo kisha unatuma kwenda namba 15551,” alisema Mateso.

Washiriki wengine sita waliobaki katika mpambano huo ni Fid Q, Chid Benz, Lord Eyez, Johmakini, Prof. Jay na Kalapina.

No comments: