Sunday, September 21, 2008

Latoya OUT! Awaaibisha Watanzania!


Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurwa amedaiwa kuponzwa na vitu vitatu ndani ya mchuano huo unaoendelea nchini Afrika Kusini.

Kitendo chake cha ‘kukandamiza malavidavi’ na Ricco wa Angola ni pointi ya kwanza ambayo ilimuondolea sifa ya kuendelea kubaki ndani ya mjengo.

Pointi ya pili ni pale aliponaswa na kamera akila denda na Moris wa Uganda, wakati huo huo mara kadhaa akawa anachojoa mbele ya wenzake, tabia ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania na Muafrika kwa ujumla.

Kufuatia hali hiyo, Latoya atatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kuchafua ‘hali ya hewa’ ndani BBA ambayo ilisafishwa vizuri na Mwisho Mwampamba mwaka 2003 na Richard Bezuidenhout mwaka jana.

Pamoja na hivyo Jumamosi iliyopita, Latoya alionesha uzalendo wa kutosha kwa kuzifagilia baadhi ya kazi za wasanii, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Joseph Haule ‘Prof. Jizze’ ambazo zilionesha kumpagawisha kwa sana.

chumba maalum walimowekwa na Tawana wa Botswana wakati wakisubiri mmoja wao kutoka, akiweka CD zenye nyimbo za wasanii hao na kucheza kwa hisia.

Mbongo huyo ambaye kwa upande mwingine alionekana kama amekumbuka nyumbani alianza kupagawa na ngoma za Mwana FA, ikiwemo inayotamba hivi sasa, ‘Bado Nipo nipo’, kisha akabadilisha na kuweka CD yenye nyimbo za Profesa Jay, kitu ambacho kilimfanya apandishe mzuka zaidi wa kucheza na kuimba, hasa aliposikia kazi kama ‘Hapo Vipi’, ‘Ndivyo sivyo’ na ‘Nang’atuka’.

Pamoja na mabaya yote aliyoyafanya mjengoni humo, safu hii inampa ‘big up’ za kutosha Latoya kwa kuonesha uzalendo huo wa kuzifagilia na kuzipa promo kazi za Wabongo wenzie. Wakati huo huo, mshiriki kutoka Kenya, Sheila anaendelea kupeta kimapenzi na Takondwa ‘TK’, kitendo kinachowafanya washiriki wengine wakae wakinong’ona juu yao.

6 comments:

Anonymous said...

jamani kila kitu molandio muandikaji na asiekubali kushindwa si mshindani.na pia mkumbuke mshafika ukomara 2basi sasa ni zam ya wengine sio rizki tusikae kumjadiliiiiiiiiiiiiii kama kaua mtu ni yeye mwenyewe ndie aloamua kushiriki.walokwenda olmpict
y wamefika wapi nao ni bahati ya m¨tu tushukuru tu amerudi salama basi

Anonymous said...

Peoples
Latoya has just been evicted but let me tell you that for a secretary,Latoya is very intelligent and just too smart. She is good for thecameras and knows what to say where. Guys, Latoya, for your average Tanzanian secretary, she is very good.Guys lets maintain the spirit but Latoya rocked. Haki without a doubtshe rocked.

Anonymous said...

Hamna kitu mbumbumbu huyu mi nlijuwa hana round ndani ya BBA! IQ yake ndogo sana! Huwezi ukaka mbele ya camera uka expose strategies zako. Yeye anakuwa na uhusiano na wanaume 2 ndani ya wiki 1, kisha anaeleza mbele ya camera kwamba hana mpango na hata mmoja wao ila anataka ku "make" "drama"! Hivi anaakili huyu? Au haelewi kwamba wanaoamuwa kum'bakisha ndani ya BBA ni wapiga kura kutoka nchi 13 na sio Tanzania pekee! Sasa kama unawatangazia wapiga kura wa uganda na Angola kwamba unataka kuwachezesha tu washiriki wao kwa faida yako, hivi unafkiri wataku support? Kwa maana hiyo tayari kura 2 ushapoteza! Na kwenye eviction unasimama na washiriki wengine sio hao (uganda na angola) kwa hiyo unajiongezea idadi ya maadui! Tanzania kura yake ni moja tu!

Vile vile kwa upeo wake mdogo wa ufahamu, ameshindwa kuelewa kwamba sio kila strategy ina "work" kila mtu na kwa kila sehemu! Strategy yake ya kujirusha, kwa jamii ya ki afrika inatafsiriwa tofauti akifanya mwanaume na pindi anapofanya mwanamke! Ndo maana Richard alipata nafasi nzuri (ushindi)kuliko Tatiana, ingawa wote walifanya upuuzi 50% by 50%. Hiyo ilitosha kumuonesha njia Latoya, lakini hakuwa na uwezo wa kung'amuwa, nae akadesa (akaiga) upuuzi ule ule, hovyooooooooooooo kama mchuzi wa magozi!!!

Halafu anasauti inakereketa masikioni (mbayaaaaa)! Afadhali ametolewa anajifanya "much know"! Tanzania tuna utu wetu, dada zetu bado wanastaha zao, hawajafikia hatua yakukaa mbele ya TV 24 HRS,wakikandamizana na wanaume walokutana nao ndani ya siku 7 tu! Hata kama nikutafuta hela dada yako ilizidi, sasa kaigize "porn" ndo lililobaki!

Anonymous said...

Amejitahid sana, ila bahati haikuwa kwake pale wenzake walipoamua kumchagua atoke kwa kuwa alikuwa anapambana na "Strong contenders" Lakini kama angekuwa amewekwa na Haze, Lucille au TK, for sure angewashinda na kubaki kwenye nyumba.

Anonymous said...

jamani huyu dada hakumuaibisha mtanzania yeyote kuna nini cha ajabu amefanya jamani???? kama kiss mbona lucile ameskiss na TK kwa raha zao na hawakutoka???? na hayo malividavi mbona Sheila na TK wanaendelea kwa raha zao. watanzania wengi hawajui kananu za mchezo.Latoya alikuwa tishio ndani ya nyumba hivyo ni mikakati ya washiriki wenzake na nchi nyingine kumtoa ili tanzania isishinde tena.

Anonymous said...

Latoya ur my hero come back home baby, ur beautiful n intelligent.