Wednesday, June 10, 2009

'Ndoa ya Obama Ilikuwa Chupu Chupu Kuvunjika Mwaka 2000' Inbox X Reply to all Forward Reply by chat Filter messages like this Pri

Rais Obama na Mkewe enzi zao za ujana

Imegundulika kuwa ndoa ya rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle ilikuwa kwenye mashaka ya kuvunjika mwaka 2000 baada ya Obama kupigwa mwereka kwenye uchaguzi wa kongresi.Kwa mujibu kitabu cha "Renegade: The Making of a President" cha mwandishi wa Marekani Richard Wolffe, rais Obama mnapo mwaka 2000 ilimbidi atenge muda wa kuokoa ndoa yake baada ya mashaka makubwa kuingia kwenye ndoa hiyo kufuatia Obama kupigwa mwereka kwenye uchaguzi wa Kongresi.

Michelle alikuwa akimlaumu Obama kwa ubinafsi kwa kujali sana mambo ya siasa na kutumia muda wake mwingi kwenye siasa badala ya familia yake.

Obama naye alikuwa akimlaumu Michelle kwa kuwa mtu baridi na kutokuwa karibu naye kwenye mambo yake.

"Katika kipindi hicho mapenzi yalipungua na kulikuwa hakuna maelewano mazuri" kilisema kitabu hicho. Inasemekana kwamba wapenzi hao walikuwa hawakai pamoja kupiga stori karibia mwaka mzima kutokana na mgogoro huo.

Uchachu huo katika ndoa hiyo ulitokea kipindi ambacho mtoto wao wa mwisho Sasha alizaliwa.

"Michelle alikuwa akiona siasa ni kama mchezo wa kupoteza muda tu" kilisema kitabu hicho.

Utulivu ulirudi katika ndoa yao baada ya Obama kuchaguliwa kuwa seneta mwaka 2004.

Yona Fares Maro
I.T. Specialist and Digital Security Consultant________

1 comment:

Anonymous said...

we yona acha wizi
habari umeitoa nifahamishe.com unaipa jina lako chini