Friday, August 7, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Chameleone amjaza mimba nyingine mkewe
The wonderful vocalist from UG, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ ameonesha uwezo katika sanaa ya kujaza watu duniani, baada ya kumpachika mimba nyingine mkewe, Daniela Atim.

Ijumaa Showbiz inakujulisha kuwa hivi sasa Chameleone anatarajia kupata mtoto wa tatu kutoka kwa Daniela ambaye mpaka sasa amekwisha give birth mara mbili watoto wa kiume, Abba na Alfa Mayanja.

Mbali na hilo, hivi karibuni Chameleone alizindua mfuko wa kusaidia watu wasiojiweza kwa kushirikiana na makampuni mawili ya vinywaji pande za UG, Nile na Crown Beverages.
*****************************************

Hii ni Dar mpaka Moro, Dom
Baada ya kuangusha shoo kadhaa za utambulisho wa albamu tatu kwa mpigo katika mikoa ya Rukwa, Mbeya na Iringa, makundi mawili ya muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume Family na Tip Top Connection yaliyoungana na kupiga kazi pamoja sasa yanageuzia mashambulizi Morogoro na Dodoma.

Akipiga stori na safu hii memba wa TMK, Said Juma ‘Chege’ alisema kuwa mizuka imeshapanda kwa ajili ya kusababisha Moro ambako zitatambulishwa albamu nne, Mtoto wa Kichaga ya Amani James Temba ‘Mh’, Pesa ya Hamad Ally ‘Madee’, Ripoti Kamili ya Tundaman na Spark bila kuiweka kando, Mkubwa na Wanawe ya Said Fella ‘Mkubwa’.

Chege ambaye amesimama vilivyo katika wimbo Running Roll ambao amepewa featuring na mwanadada Wahu, alisema kuwa katika ziara hiyo ambayo wameipa jina la Wanaume Family na Tip Top Kazini Tour, wakiwa Moro watakamua kwenye Ukumbi wa Bwalo la Umwema na baadaye Uwanja wa Jamhuri.

“Siku inayofuata tutadondoka Dom ambako nako tutasimamisha mizuka kwenye Uwanja wa Jamhuri,” alisema Chege ambaye katika wimbo huo aliofanya na Wahu, ameonesha kiwango cha kijanja.
*****************************************************

Exclusive: K-Sher avuta mkoko mpya
Hii ni exclusive, mwanadada wa Bongo Flava, Khadija Shaaban ‘Keisha’ hivi sasa atakuwa adimu kwenye vituo vya madereza tax kama ilivyokuwa zamani na kwenye daladala ndiyo kabisaaaa!

Iko hivi, Keisha ambaye ni mwanamuziki bora wa kike 2008-09, kwa mujibu wa Tuzo za Dandu, ametungua ndinga mpya aina ya Toyota Vitz na akikatiza nalo kitaani utalishuhudia likiwa na rangi nyekundu huku namba zake za usajili zikisomeka T 771 BBK.

“Nimeipenda sana plate no. yangu, ile BBK ni kirefu cha Baby Keisha,” alichonga Keisha kwa mapozi. Hey Baby Keisha, u deserve congratulation mama, ndo' ustaa wenyewe wa kibongo!
**************

Wasanii wanaotarajiwa kupiga kazi ndani ya muvi ya Tears On Valentine iliyoandaliwa na Kampuni ya Tollywood Movies wamemaliza mazoezi ya nguvu (kama wanavyoonekana pichani) na wanatarajiwa kuanza shooting wiki ijayo na wameahidi kutoa muvi kali kuliko zote.
*****************************

Ijumaa Sexiest Bachelor
Ni mchuano wa kijanja, guys wenye mguso wa kimahaba ndiyo wanaoshindanishwa hapa. Msanii Steven Kanumba, ambaye kwa sasa anatamba na sinema yake mpya ya The Director, ndiye anayeshikilia taji la Ijumaa Sexiest Bachelor na mwaka huu amependekezwa tena kuingia shindanoni.

Kazi yako ya awali uliyotakiwa kuifanya umeitekeleza ipasavyo. God bless u! Kupitia kura uliyoidondosha kwetu, tumeweza kupata orodha ya kukata na shoka ambayo inakuijia hapo chini.

Unachonatakiwa kufanya ni kupiga kura ili tubakize watu 12 wiki ijayo. Inawezekana Mtanzania. Angalia majina kwa makini kisha tuma kura yako kwenye simu namba 0787- 110173 ukimtaja mtu ambaye unadhani anastahili kuendelea kuwepo shindanoni.

Majina ni haya; Hemedi, Marlaw, Gwamaka Kaihula ‘Gk’, Steven Kanumba, Yusuf Mlela, Vincent Kigosi ‘Ray’, Adamu Mchomvu, Mwisho Mwampamba, Kalapina, Dudubaya, P. Funk, Shija, Black Rhino, Mb Dog, Tundaman, Benn Kinyaiya, Spark, Dully Sykes, Chid Benzi, Tino, Jumbe Yusuf, Jerry Tegete, Ally Mustafa, Chege, Makamua na Mr. Blue.
Wengine ni AY, MwanaFA, Ally Mustafa, Henry Joseph, Hessein Machozi, Fid Q, Niki wa 2, Hermy B, Jay Moe na Johmakini.
*************************

1 comment:

Anonymous said...

nyie kwa kubofoa bwana i Bachelor sio barchelor rekebisha upesi.