Monday, September 7, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Mkubwa na ngoma mpya
Bosi wa crew ya TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’ anazidisha harakati zake kwenye muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava na hivi juzi ame-release ngoma mpya yenye jina la ‘Tunapambana’. Fella alichonga na kona hii kisha kuijuza ya kwamba dude hilo ambalo limewashirikisha wanawe, TMK Family ni moja ya songs zilizomo ndani ya albamu yake ambayo inapaa kitaani hivi sasa kwa jina la Mkubwa na Wanawe.

Mkubwa ambaye ali-exist katika game long time ago kama meneja wa wasanii, hivi sasa ameongeza mwendokasi kiaina kwa ku-manage artists na kushika MIC kwa wakati mmoja ambapo traki yake ya kwanza inavuta pumzi kwa jina la 2008-2009. ********************************

KIM: Ameshea utamu na midume 8
Ni kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa staa wa kike nchini Marekani, Kim Kardashian especially katika eneo la idadi ya wanaume ambao ameonja nao utamu. Mtandao ambao ume-specialize katika kumulika jinsi mastaa wa kiwanja wanavyobadili wapenzi, unaweka kweupe kwamba mdada huyo amewahi kujiachia na wanaume wanane.

Damon Thomas anatajwa wa kwanza ambapo walijikunja kati ya mwaka 2000 – 04, mwaka 2005 hakuona soo kuchangamsha damu na vocalist wa rhythm laini, Kenneth Edmonds ‘Baby Face’. Mdogo wake Brandy, Ray-J naye alionja naye tamu mwaka 2006, mwaka ambao pia Nick Lachey, Benji Madden na Nick Cannon walimmega kisela. Cannon alitemana na Kim mwaka 2007, kisha kuangukia kwa Reggie Bush ambaye waliachana mwaka 2009.

Mwaka 2008 wakati akiwa na Reggie Bush, pia hakusita kukwea on bed na Devon Murray, hivyo kuifanya idadi ya wanaume walio-make CV ya kuwa naye faragha kutimia wanane.
***************************


Madhila 2 bado siku 7
Filamu ya Madhila ambayo inatajwa kuwa na stori ya kusikitisha, inayobeba uhalisia wa maisha ya walemavu kwenye jamii ya Watanzania, ipo njia moja kwani imebakiza siku 7 a.k.a one week only ili iingie kitaani.


Filamu hiyo inayosambazwa na kampuni mkombozi wa vipaji nchini, Tollywood Movies, inaelezewa kuwa i imezingatia thamani halisi ya kiwanda cha filamu Bongo. Habari kutoka Tollywood zinasema kuwa kila kitu kuhusu ujio wa Madhila II kitaani kimekamilika, hivyo Watanzania wanatakiwa kukaa mkao wa tayari kujipatia nakala kupitia DVD, VCD na VHS.
*************************************

compiled by mc george

No comments: