‘Kufanya diet’ hakuna maana ya mtu kujinyima kula vyakula unavyovipenda na kujikondesha, bali ni wewe kuwa huru kufurahia mlo unaokula, kuwa na nishati ya kutosha mwilini, kuendesha shughuli zako na kula vyakula vya aina mbalimbali vya kujenga na kulinda mwili wako dhidi ya maradhi.
Kuyafanya yote hayo kunahitaji elimu ya kutosha juu ya vyakula unavyopaswa kula kila siku na kuachana na ile dhana potofu kuwa kufanya ‘dayati’ maana yake ni kula kiasi kidogo cha chakula. Unahitaji kujua misingi ya virutubisho vya vyakula na kuvila kwa mpango unaokufaa.
Katika makala ya leo, tunaangalia kanuni ya ulaji vyakula na tutajifunza aina ya vyakula tunavyopaswa kula ambavyo husaidia kulinda miili yetu na vile ambavyo huchangia miili yetu kupatwa na maradhi.
Kanuni ya kwanza inahitaji mtu kujua mahitaji ya mwili wake na kula kiasi kinacholingana na mahitaji ya mwili. Hapa mtu anatakiwa kula kiasi kinacholingana na uzito wa shughuli unazozifanya kila siku.
Kila unachokula kinajulikana kama ‘calories’ na kwa wastani mtu mzima anatakiwa kula kiasi cha ‘calories’ zisizozidi 2000, pia inategemea umri, uzito na urefu wa mtu.
Kula ‘calories’ nyingi na kufanyakazi kidogo ni sawa na UNENE. Kula ‘calories’ kidogo na kufanya kazi nyingi ni sawa na WEMBAMBA. Kula ‘calories’ zinazolingana na kazi unazozifanya ni sawa ‘KUDUMISHA UZITO ULIONAO’.
Kula mchanganyiko wa vyakula
‘Dayati’ ni kuongeza wigo wako wa kula vyakula mchanganyiko vyenye virutubisho, hususan mbogamboga, nafaka na matunda, hata yale usiyoyala mara kwa mara.
Kula kiasi cha wastani
Epuka ulaji wa kushiba kupita kiasi, hasa ulaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ‘calories’, badala yake pendelea kula kwa wingi matunda, mbogo za majani, vyakula vyenye kiwango kidogo cha mafuta, vyenye mafuta na chumvi kidogo. Hakikisha pia unapata vyakula ‘Fresh’ na asilia zaidi.
Kunywa maji mengi
Asilimia 75 ya mwili wa binadamu ni maji, hivyo kunywa maji ni sehemu muhimu sana ya ‘dayati’. Maji husaidia sana kusafisha mifumo ya miili yetu, hususan figo na kibofu, kwa kuondoa uchafu na sumu. Watu wengi hupatwa na maradhi mengi kwasababu tu ya kutopenda kunywa maji mengi kila siku.
Epuka vyakula vya sukari
Punguza kiwango cha sukari unachokula kwa kuepuka ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi, kama vile soda ambayo inaelezwa kwamba ukinywa soda moja tu kila siku, kwa mwaka mmoja, unaweza kuongezeka uzito kwa zaidi ya kilo 10!
‘Kufanya dayati’ hakukusudiwa kukunyima uhuru wa kula vyakula uvipendavyo, ila unatakiwa uvile kwa wastani, huku mlo wako mkubwa ukitawaliwa na vyakula vyenye virutubisho na vitamini zaidi, kwa kufanya hivyo vyakula vingine haviwezi kukuathiri iwapo utavila kwa uchache na hiyo ndiyo inaitwa ‘balanced diet’.
Mwisho, zingatia suala la ‘ku keep busy’ mwili wako kwa kujishughulisha, ikiwemo kufanya mazoezi ya mara kwa mara. Ukizingatia hayo utakuwa na afya njema na utakuwa huna mwiko wa kula baadhi ya vyakula, kila chakula kwako kitakuwa halali na kisichokuwa na madhara yoyote.

4 comments:
ASANTE TENA KAKA KWA KWELI MADA ZAKO MI NANUFAIKA NAZO SANA
ASANTE
SCHOLA
Asante ndugu kwa makala zako zene kujaa elimu!!Leo mimi nina swali nina ndugu yangu amepata ugonjwa wa Kiharusi naomba msaa wenu hapa ni hospitali gani nimpeleke hapa bongo?au ni tiba gani natakiwa kumfanyia nikiwa nayo nyumbani?nimejaribu waganga imeshindikana,na anakuwa mkali anawafukuza anasema wanamuumiza wengi wao humlazimisha kumchuwa na kumlazimisha atembee, wakati hana uwezo huo,nitashukuru kwa ushauli wenu,asante.
hi.mimi nataka kujua jinsi ya kupunguza unene...na je kama ni wa kurithi unaweza kupungua??
suala la kupunga unene tumeshalizungumza sana humu, search makala za nyuma utaona. kifupi fomula ya kupunguza unene ni kula kidogo, kufanya mazoezi/kazi nyingi. au kwa maneno mengine ingiza kidogo toa kingi mwilini.
asante
Post a Comment