Monday, March 29, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

 Justin Timberlake: Aanza ngono akiwa na miaka13, ampitia Rihanna
Mapenzi na umri, haivutii kuyawahi ingawa marehemu Aaliyah aliwahi kutoa kibao chake, Age aint nothing but a number, alifanya hivyo baada ya serikali ya Marekani kumpiga stop kuolewa na R. Kelly, alikuwa bado binti mdogo halafu akawa anamtaka mtu mzima. Ebwana Dah!

If you had perception kwamba dogo Chris Brown alifanya mbaya kumbonda Rihanna, unaweza kuongezea na hili kuwa mbali na kasoro nyingine ikiwemo ile ya kumuambukiza gonjwa la zinaa, pia mtoto huyo wa kike alimsaliti mshkaji kwa kutoa penzi kwa Justin Timbelake mwaka jana. Site ya kiwanja ambayo ipo serious katika kuanika life style za mastaa especially katika eneo la nani kapumzika kwa nani na lini ndiyo imeweka kila kitu kweupe, pia inafichua kuwa Justin alianza mapenzi akiwa na umri wa miaka 13 tu. 

Hiyo ilikuwa mwaka 1994 ambapo alianza kutoka na Danielle Ditto kabla ya kumwagana mwaka 1996 na kurukia kwa Fergie ambaye hawakudumu, akaangukia kwa Veronica Finn alikotuliza wazimu kwa miaka miwili na mwaka 1998, alihusika katika kuutoa usichana wa Britney Spears, ingawa walikuja kutofautiana na kumwagana mwaka 2002. Mwaka 2002 alipumzika kwa Jenna Dewan alipoona inatoshwa mwaka 2003 walitemana, ingawa wakati yupo na Jenna, pia alidata kimtindo kwa penzi la Janet Jackson lakini mwanamama huyo alimtoa mbio alipoona dogo anajenga mazoea ya kukolea. 

Mwaka huo huo wa 2002, pia alijichuja kwa Alyssa Milano, mwaka 2003 akaangukia kwa Staci Flood, hakukaa, akatua kwa Cameron Diaz ambaye walizubaishana kwa miaka mitatu kisha akahamia kwa Scarlett Johansson, akamega kisela. Tangu mwaka 2007, Justin a.k.a TJ, aliangukia kwa Jessica Biel na amejituliza mpaka leo, ingawa mwaka jana (2009), alisaliti na kwenda kuchangamsha damu na Rihanna. Jina lake kwa kirefu ni Justin Randall Timberlake, alizaliwa Januari 31, 1981, Memphis, Tennessee, Marekani, umri wake ni miaka 29. Dini yake ni Mkristo na nyota yake ni Ndoo (Aquarius).
******************* 

Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA), kazi imeanza
Nominees wanaowania Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA) wapo wazi, tofauti na miaka mingine, awamu hii imekuwa ni uteuzi wenye akili kwa sababu walioshindanishwa ni wale ambao walifanya vizuri mwaka 2009 bila zengwe. Big Up One Plus, Digital Arts na wadhamini kwa kuleta mabadiliko makubwa. Ile harufu ya wasanii kususia, tayari imetoweka. Hawa ni baadhi ya mastaa wanaowania tuzo kwa mwaka 2009-2010. Listi zaidi wiki ijayo.
**************************************

Master J: Aichambua Bongo Flava to the next level
Baada ya kufanya interview na producer mwenye a.k.a nyingi kwenye game la muziki, Joachim Kimaryo ‘Master J’, tuliahidi kuyatoa maelezo yake katika matoleo matatu, wiki iliyopita tulianza na kile kinachosababisha washindi wa BSS wasifike mbali, leo tupo na Bongo Flava.

Wadau wanasema Bongo Flava inakufa, J a.k.a Baba Nuru, analizungumziaje hilo? Anachambua: “Ni kweli Bongo Flava ilikuwa inakufa kwa sababu wasanii walikuwa wanatoka nje ya mstari lakini kama mtu ni mfuatiliaji ataona mabadiliko. “Bongo Flava inarudi upya, miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti kabisa.

Wasanii wanaoingia studio kufanya kazi wanakuwa na vipaji vya kweli, kwahiyo hata kazi zinazofanyika hivi sasa zinakuwa na ubora wa hali ya juu. “Siku chache huko nyuma maprodyuza wenye viwango vidogo walituangusha, walishindwa kuzalisha kazi zenye kiwango ndiyo maana muziki wetu ukaanza kuporomoka, kwakuwa waliwatengeneza wasanii wasiokuwa na vipaji. 

“Kitu kingine ni kwamba siku za nyuma maprodyuza walikuwa wachache, ladha ikawa ni ile ile lakini siku hizi vichwa vipya vimeibuka, vina mawazo mapya na kuweka vionjo vya aina vya kuunaksi muziki wetu, hiyo imenifanya mimi kukaa pembeni na kuiachia damu changa, Marco Chali. “Kwahiyo tunakwenda mbele, Bongo Flava inakua, inakwenda level nyingine. 

Miaka miwili ijayo tutashuhudia muziki wa ukweli unasimama. Ile staili ya kubana pua ilikosea njia, haitakuwa na nafasi tena, wanaoipa afya Bongo Flava ni wakali wenye vipaji na staili mpya za kuchana ambao ndiyo wanaotawala sasa na wengine wanakuja.” Hilo ni neno la Bongo Fleva, wiki ijayo tutakuwa na neno lake kuhusu lebo yake na wasanii anaowaongoza, studio zake na harakati za muziki kwa jumla.  Usikose kucheki hapa.                           ********************************

No comments: