Thursday, December 9, 2010

KANUMBA CHINI YA ULINZI!

The Morning Alarm ni sinema inayoonesha biashara ya madawa ya kulevya inavyofanywa kiusanii wa hali ya juu na Kanumba akishirikiana na swahiba wake Benny. Kunumba na mwenzie ni wakimbizi kutoka Kongo ambako walikuwa wakifanya biashara ya kuuza silaha kwa waasi wa nchi hiyo pamoja na kufanya biashara ya kuuza madawa ya kulevya.

Mambo yanakuwa magumu nchini mwao baada ya jeshi la polisi nchini hiyo kuwashitukia na kuanzsha msako mkali wa kuwatia nguvuni. Wanaona mambo magumu wanaamua kukimbia nchi na kuingia nchini kwa kificho.

Wanajibadilisha na kujifanya walala hoi, hawana kitu, wanavaa nguo chafu chafu na wanaishi kijimbu cha uswahilini huku wakijifanya wauza magazeti. Humo wanahifadhi baadahi ya siliha walizoingia nazo nchini na madawa ya kulevya, wanaaza kutafuta wateja taratibu na hatimaye wanapata wanunuzi wa madawa yao na hapo ndipo asakari wa Bongo wanaanza kufuatilia nyendo zao......
Kanumba na Benny wanawekwa chini ya ulinzi na mashushu wa Bongo
Kanumba na Benny wanawageuzi kibao mashushu na kuwaweka wao chini ya ulinzi
mashushu wakiwa chini ya ulinzi wa mtutu wa bastola
katika pilika zake, Kanumba anamgonja msichana na gari na kulazimika kumpeleka hospitali
wako katika mishemishe zao...Hashim Kambi kashika bahasha ndani yake kuna unga kaletewa kununua....dili limejipa....!
Benny anakutana na Machangudoa wa mjini, wanamuweka mtu kati usiku na pombe zake kichwani....pokea bahasha yako hiyo...kijana anauziwa unga na Kanumba
...sasa mtu wangu, twende wapi kwingine tukauze?
..benny amepata mteja mwingine..Maya...anakaribishwa ndani na anapewa na konyagi vile vile kupozea.... KAA MKAO WA KULA, MORNING ALARM INAKUJA MTAANI KWAKO HIVI KARIBUNI!


No comments: