Ukisikia ng'ombe hazeeki maini nd'o hii. Mzee mmoja kutoka India, Ramajit Raghav mwenye umri wa miaka 94, amemjaza mimba mkewe Shakuntala (59) na kumzalisha mtoto na kwa kitendo hicho mzee huyo amejihesabu kuwa mzee kuliko wote aliyeweza kumjaza mkewe mimba.
Alipoulizwa siri ya 'nguvu' zake katika umri huo, ambao inaaminika nguvu za kiume huisha, Mzee Raghav alisema kuwa mlo wake wa kila siku huwa ni nusu kilo ya samaki, lita 3 za maziwa na kilo moja ya samli.
Kuhusu future ya mwanae, mzee huyo alitamba kwa kusema kuwa anaamini ataendelea kumlea mwanae kwa miaka mingine kumi.
"Njoo baada ya miaka 10 kuanzia sasa na utanikuta niko hivi hivi. Nitakufa kama nitaumwa na nyoka mweusi ambaye yuko mbali sana," alitamba mzee huyo wakati akiongea na mwandishi wa mtandao mmoja.

No comments:
Post a Comment