Saturday, September 24, 2011

JUKWAA LA WAHARIRI LAPIGWA MSASA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju akifungua semina ya Wahariri wa Vyombo vya habari nchini iliyolenga kuwafahamisha kuhusu kusaidia kuandika habari juu ya haki za binadamu. Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya mahusiano ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mathew Mwamu.
Pichani Juu na Chini ni miongoni mwa Wahariri Wakuu wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada katika Hoteli ya Double Tree By Hilton jijini Dar es Salaam.
 
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akisikiliza hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju wakati wa Ufunguzi wa Semina ya siku moja ya wahariri wakuu wa vyombo vya habari (TANZANIA EDITORS' FORUM) iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam.
 Jopo la Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari wakiwa katika semina elekezi juu ya haki za Binadamu iliyoratibiwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Umoja wa Mataifa nchini.
 Pichani Juu na Chini ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akisoma hotuba katika ufunguzi wa Semina hiyo
 
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mhariri wa Makala wa Gazeti la Serikali la kila siku (Daily News) Deogratius Mushi.
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou akifanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha TBC1.(Picha by http://dewjiblog.com/) Pamoja na ufafanuzi huo, waandishi wa habari waliendelea kuwabana viongozi hao watoe ufafanuzi wakiegemea katika kitabu cha Quoran kwamba kinaeleza nini kuhusu hijab jambo ambalo liliwaudhi.
miongoni mwa Wahariri Wakuu wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa

No comments: