Monday, September 26, 2011

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE CAMBRIDGE WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU

Mgeni rasmi Hoyce Temu akiwapa risala wahitimu wa kidato cha IV katika shule ya Cambridge. Hoyce aliwasihi wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanafanya mitihani yao kwa utulivu na kujiamini sambamba na kuwasisitiza kuchagua masomo yenye masoko katika ajira na kujiendeleza binafsi. Aidha aliwaomba wazazi na walezi kuwasaidia vijana hao katika safari yao ya Maisha na kuwataka kuwa wavumilivu wakati wote ili waweze kufikia mafanikio.
Mwanafunzi Monica Mwaipopo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Hoyce Temu cha kufanya vizuri katika taaluma na Vilabu Shuleni hapo.
Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita akihamasisha uchangiaji wa fedha za Mtoto Sesilia Edward ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo anayetarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu. Mtoto Sesilia aligundulika kufuatia kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Channeli Ten na kuendeshwa na Hoyce Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hiyo.
Umati wa  wageni waalikwa, walezi na wazazi waliohudhuria mahafali hayo ya kumi na moja shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Cambridge wakiingia rasmi katika sherehe za mahafali yao kwa wimbo maalum.
Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Cambridge.

No comments: