Tuesday, October 18, 2011

JK ataembelea banda la Vodacom Mkutano wa uwekezaji

Sehemu ya mabalozi na wawekezaji wakifuatilia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) ya ufunguzi wa  kongamano la uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika uliofanyika jana mjini Mpanda. Zaidi ya wajumbe miatatu kutoka sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi walihudhuria kongamano hilo ambapo fursa za uwekezaji katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ziliainishwa na kujadiliwa kwa kina. Vodacom ilishiriki kuwezesha kongamano hilo.
Rais Jakaya Kikwete akifungua kongamano la uwekezaji katika eneo jipya la uwekezaji kanda ya ziwa Tangayika jana Mjini mpanda mkoa mpya wa Katavi. Zaidi ya wajumbe mia tatu kutoka sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi walihudhuria kongamano hilo ambapo fursa za uwekezaji katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ziliainishwa na kujadiliwa kwa kina. Vodacom ilishiriki kuwezesha kongamano hilo.
 
Rais Jakaya Kikwete akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim kuhusu mchnago wa kampuni hiyo katika kuunga mkono mpango wa serikali wa kushawishi uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika wakati rais Kikwete alipotembeela banda la Vodacom wakati wa maonesho yaliyofanyika pembezoni mwa kongamano la uwekezaji ukanda mpya wa uwekezaji ziwa Tangayika uliofanyika jana Mjini Mpanda na kufunguliwa na Rais Kikwete.Katikati ni Meneja wa M-PESA mikoa ya Ruklwa na Katavi

No comments: