Sunday, October 2, 2011

WANANCHI WAPEWA HUDUMA ZA AFYA BURE

 Banda la Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nalo halijabaki nyuma katika kutoa huduma bila malipo kwa wananchi wanaotembelea maadhimisho yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni Shamra shamra za kusheherekea miaka 50 ya  Uhuru ya Utoaji Huduma za Afya Tanzania. Pichani ni Dkt Fidelis Mgohamwende akichukua vipimo vya damu kwa mmoja wa wananchi.
 
Katika siku ya pili ya maadhimisho ya utoaji huduma za Afya Tanzania tangu Uhuru Wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Kitengo cha Uchunguzi wa Awali wa Saratani ya Kizazi Wauguzi Maria Haule (kulia) na Genoveva Mlawa wakitoa huduma na maelezo mbalimbali kwa mmoja wa kinamama aliyejitokeza kuchunguza Afya yake.
Dkt. Neema Ijani na Dkt. Jennifer Raymond wakiongea na binti aliyefika katika banda la Uchunguzi wa Saratani ya Matiti kuchunguza Afya yake.
Baadhi ya wananchi wakisubiri katika foleni ya kupata huduma ya Bure ya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Matiti kwa kina Mama.
Afisa Mdhibiti Ubora kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Winfrida Mrema (kulia) akimfanyia vipimo mwananchi aliyefika katika banda hilo kwa ajili ya kujua afya yake.

No comments: