Monday, October 24, 2011

MAONYESHO YA MCHEZO WA KAPOEIRA @ RUSSIAN CULTURAL CENTRE

Mwalimu wa Mchezo wa Kapoeira ambao ni utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil Mestra Janja akizungumzia umuhimu na faida za mchezo  huo kwa wageni waliohudhuria Onyesho la mchezo huo katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapoelista Gabriel Limaverde ambaye alikuwa akitafsiri Ujumbe huo kwa Lugha ya Kingereza. 

Mestra Janja amefafanua kwamba Kapoeira ni Utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil na Alama madhubuti ya Wabrazil, hazina Muhimu ya Utamaduni wa Utu na Umoja na ni Sanaa ya Kibrazil ya Ulinzi na Kujikomboa kutumia akili na viungo vya kibinadamu. Pia ni sehemu ya taaluma, fani na ujenzi maalum nchini Brazil na nchi zingine ambako imekubalika na kutambulika, hivyo inafundishwa na inachezwa katika nyanja mbalimbali na kuzingatiwa katika tafiti za viwango tofauti vikijumuisha na  vya Shahada ya Uzamili (Master's Digrii) na Digrii ya Udaktari wa Falsafa kwenye masomo ya Anthropologia, Historia, Soshologia, Elimu na Elimu ya Viungo

Wadau wakifuatilia kwa umakini
Picha za Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa

No comments: