Wednesday, October 26, 2011

MRADI WA VODACOM"MWEI"JINSI UNAVYOINUA WAKINAMAMA NCHINI TANZANIA

Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa  akiongea na wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,kabla ya kuanza kuwapatia  mikopo ya fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake  wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini na kurudisha fedha hizo bila riba.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakimsikiliza Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa (hayupo pichani) ,wakati  wakisubiri kupatiwa mikopo yao ya  fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakiwa wameketi wakisubiri kupatiwa mkopo wa fedha taslimu unaotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa  akimpatia Mwanaidi  Musa  mkopo wa fedha taslimu      kwa ajili ya kufanyia biashara zake na kuzirudisha fedha hizo bila riba yoyote,aliyekaa kushoto ni Mratibu wa Mfuko huo Ally Mbuyu.

No comments: