Ngoma Africa band kupewa Tuzo la kimataifa,
" IDA - International
Diaspora Award"
Habari za uhakika zinatonya kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" au
maarufu kwa jina la "FFU" wazee wa virungu na makombora ya muziki,yenye makao
yake nchini Ujerumani, Bendi imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki ya Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu la " IDA - International Diaspora Award" award hiyo inatolewa
na tahasisi za kimataifa,itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo
Kamanda Ras Makunja wa FFU siku ya Jumapili ya 12-8-2012 katika sherehe maalu za Gala night zitakazo udhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo mastaa.
Inasemekana Sherehe za kukabidhiwa tuzo hiyo zitafanyika mjini Tubingen, mkoa wa Baden württemberg, kusini mwa
ujerumani.
Tahasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika inayolitangaza bara la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia ushindi wa mamlioni ya kura, pia
imegundulia kuwa bendi
hiyi inakubalika na
mamilioni ya washabiki wa
mataifa mbali mbali, Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni
50 duniani kote,hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa, kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya washabiki,ni bendi ambayo kipenzi cha mamilioni ya washabiki. katika kambi yao hii www.ngoma-africa.com inakadiliwa kuwa na mamilioni ya lank.
Tunawatakia kila yaliyo mema FFU wetu www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment