Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini wakiwa wamekusanyika katika shule ya Msingi Tandale jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyakazi za kujitolea kwa dakika 67 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 mwezi Julai.
Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mh. Ibrahim Mukiibi akiwasili kushiriki zoezi hilo.
Mabalozi wa Afrika Kusini Mh. Henry Chiliza (kushoto) na Mh. Ibrahim Mukiibi wa Uganda wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wakisalimiana baada ya kukutana katika zoezi la kujitolea kufanya kazi za kijamii katika shule ya msingi Tandale ya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joymrey Von de Merwe.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa namna ya kutekeleza zoezi hilo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa baada ya kuweza kukarabati madawati yalioharibika, kupiga rangi Ubao za kuandikia madarasani na kufanya usafi katika mazingira ya shule hiyo.
Bi. Stella Vuzo amesema katika kuadhimisha siku kama hii mwaka jana Umoja wa Mataifa ulitoa huduma za Kibinadamu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Saratani na mwaka huu wameonelea ni vyema kuungana na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale kwa kuonyesha wanajali na kutoa huduma kama hizo katika shule hiyo chini ya kauli mbiu ya mzee Nelson Mandela "Inspire Change Within Your Self".
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete (katikati) akitoa shukrani kwa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini ambapo ameelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili shule zikiwemo Uhaba wa Madawati, Vyoo, Ubovu wa Sakafu za Vyumba vya Madarasa na kuwaomba wadau kujitokeza kuwasaidia ili kuboresha mazingira mazuri kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kutoka kushoto ni Kansela wa Masuala ya Siasa Bw. Terry Govender na Joymery Von De Merwe kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete.
No comments:
Post a Comment