Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akimkabidhi barua Mwanafunzi wa kidato cha nne wa
Shule ya Sekondari Azania Rahim Rajab ambaye ni mmoja wa kati ya
wanafunzi wawili wajumbe wa UN Clubs waliochaguliwa kuhudhuria Kongamano
la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela litakalofanyika Johannesburg Afrika Kusini ambayo
huadhimishwa kila mwaka Julai 18.
Wanafunzi hao wamepewa duhamini wa Tiketi za kwenda na kurudi na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways-SAA).
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akimkabidhi barua ya kuchaguliwa kushiriki Kongamano
hilo Afrika Kusini Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa Nuru Kessy ambaye ni Mwanachama wa Un Clubs.
Bw.
Phillippe Poinsot (kulia) akimfafanulia Mwanafunzi Nuru Kessy kuwa
katika Kongamano hilo watakutana na wanafunzi wenzao kutoka mataifa
mbalimbali duniani wenye umri kati ya miaka 13-18 na kuwa wanahitaji
kufanya utafiti kuhusiana na maisha ya Mandela ikiwemo miaka ya mwanzo,
maisha yake ya jela, maisha ya uraisi kama mtu aliyepokea tuzo ya Amani
ya Nobel, kustaafu kwake na mchango wake kama kiongozi maarufu duniani.
Wanafunzi
hao wakitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot (kulia) na Head, Management
Support Strategy and Partnership wa UNDP Ishmael Dodoo (kushoto).
Wanafunzi
ambao ni wanachama wa UN Clubs wanaoelekea Afrika Kusini katika
Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Nelson Mandela kwa
udhamini wa shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) katika picha ya
pamoja na Wafanyakazi wa UNDP. Kushoto ni Reference Assistant kutoka
kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Harriet Macha, IT Associate
Alice Chopeta, Head, Management Support Strategy and Partnership wa
UNDP Ishmael Dodoo, Wanafunzi Rahim Rajab na Nuru Kessy, Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe
Poinsot na Information Officer UNIC Stella Vuzo.
No comments:
Post a Comment