Monday, January 27, 2014

PROIN GROUP OF COMPANIES YAFANYA SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA 2014 NDANI YA MJENGO WA TRANIC PLAZA MWISHONI MWA WIKI

  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies Bw Johson Lukaza akiwakaribisha wafanyakazi wa makampuni yaliyo chini ya Proin Group of Companies pamoja na wageni waalikwa katika sherehe ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Jengo la Kampuni hiyo la Tranic Plaza.
Mshereheshaji wa Sherehe hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria sherehe hiyo ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza


Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya kukaribisha mwaka 2014 iliyoandaliwa na Proin Group Of Companies wakigonga glasi kama ishara ya Upendo na Kuupokea mwaka katika sherehe iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza

 Baadhi ya wakurugenzi wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies wakikata keki Kama ishara ya kuukaribisha Mwaka 2014 kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Jengo la Tranic Plaza.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Infinity Communication Stella Sakia akitoa Maneno ya Ukaribisho kwa Wafanyakazi wote walio chini ya Proin Group of Commpanies na wageni waalikwa wote katika sherehe ya kuukaribisha mwaka iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini kila tukio lililokuwa likiendelea katika sherehe hiyo
 Raha ya sherehe ni Msosi na Mziki baada ya hapo.........
 Baadhi ya wafanyakazi kutoka Proin Promotions Limited kampuni moja wapo iliyopo chini ya Proin Group Of Companies wakiwa katika pozi la picha
Haya Baada ya Msosi wadau wakiserebuka Kwaito...
Mmiliki wa mtandao wa Lukaza Blog, Bw Josephat Lukaza akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kukutana katika Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

No comments: