Monday, February 24, 2014

TAMASHA LA PASAKA 2014 KUJA KIVINGINE

Tamasha la pasaka la Mwaka huu litakalozinduliwa rasmi April 20,jijini dar likibeba kaulimbiu ya "Tanzania kwanza haki huinua Taifa",litaemdendeshwa kwa namna ya Wadau wenyewe kuchagua waimbaji,aidha iwe kutoka ndani ama nje ya nchi ikiwemo sambamba na mgeni rasmi.

Hayo yalibainishwa jijini Dar,mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions,ambao ndio wandaaji wa tamasha.Alifafanua kuwa wapenzi wa muziki huo ndio watakaochagua waimbaji hao kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba 15327, kwa kutumia mitandao yote ya simu.

"Tamasha la mwaka huu linakuja kwa mtindo wa kipekee kabisa,ambapo wapenzi wa muziki wa injili watakuwa na fursa ya kuwachagua wanamuziki watakao penda waje kutumbuiza ikiwemo na Mikoa litakapo fanyika tamasha hilo, tofauti na miaka mingine na wale wote watakao pendekezwa tutawaleta kutoa burudani",alisema Msama.

Alisema,licha ya kuweka utaratibu huo,kumekuwa na changamoto kubwa kwa wapenzi hao wa muziki wa injili ambao wanataka wanamuziki waliotoa burudani wakati wa tamasha la krimasi akiwamo Solly Mahlangu kutoka nchini Afrika Kusini.

Msama alisema,maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na katika mazingira ya kwenda na wakati,limekuwa  na kauli mbiu ya "Tanzania kwanza haki huinua Taifa".


Miongoni mwa waimbaji waliotikisa tamasha la Krismas ambalo lilizinduliwa rasmi Desemba 25,mwaka jana jijini Dar,kabla ya kuhamia mikoani,Ni Solly Mahlangu,Ephrahim Sekereti,Rose Muhando,Upendo Kilahirio,Upendo Nkone,Edson Mwasabwite na wengineo,wakiwemo vijana wa Acapella a.k.a The Voice.

No comments: