Friday, February 26, 2016

Shinda Nyumba, Mshindi wa Pikipiki Akabidhiwa

SHINDA NYUMBA (10)Afisa Masoko Msaidizi wa Global Publishers, David Mwaipaja (kulia) akimkabidhi Lucy Swai ufunguo wa pikipiki aliyoshinda kwenye droo ya pili ya Shinda Nyumba, hafla imefanyika leo kwenye Ofisi za Kampuni ya Global Publishers, Bamaga Mwenge - Dar.SHINDA NYUMBA (6)
David Mwaipaja (kulia) akimkabidhi Lucy Swai ufunguo wa pikipiki aliyoshinda.SHINDA NYUMBA (2) Robert Wilson akipokea king’amuzi na dishi kutoka kwa mwakilishi wa Ting, Betty Bonzon.
SHINDA NYUMBA (4)Betty Bonzon akikabidhi zawadi kwa mshindi.SHINDA NYUMBA (5)Afisa Usambazi wa Kampuni ya Global Publishers, Jimmy Haroub (kulia) akimkabidhi simu ya kisasa Emmanuel Henry wa Dar aliyoshinda katika droo ya pili. SHINDA NYUMBA (1)Betty Bonzon akikabidhi zawadi ya king'amuzi cha Ting kwa David Nasali aliyemwakilisha mwanaye Agnes Pallangyo wa Singida ambaye alishindwa kufika kwenye hafla hiyo. SHINDA NYUMBA (3)Betty Bonzon akikabidhi zawadi ya king'amuzi cha Ting kwa Thomas Kilala wa Arusha.SHINDA NYUMBA (8)David Mwaipaja akiwapongeza washindi wa droo ya pili ya Shinda Nyumba kuhimiza wasomazji wa Magazeti ya Global waendelee kushiriki shindano hilo. SHINDA NYUMBA (11) Lucy Swai akiwa amepanda pikipiki aliyoshindaSHINDA NYUMBA (12) Lucy Swai akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi wa pikipiki.SHINDA NYUMBA (13)Jimmy Haroub (kulia) akimkabidhi vyombo vya jikoni, Francisca Mlalo baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili. SHINDA NYUMBA (16)Francisca Mlalo akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili. SHINDA NYUMBA (22) Picha ya pamoja ya washindi wa droo ya pili ya shindano la Shinda Nyumba.
DAR ES SALAAM: Shindano la Shinda Nyumba linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Limited kupitia magazeti yake ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi limezidi kunoga baada ya washindi waliotangazwa kwenye droo ya pili kukabidhiwa zawadi zao akiwemo Afisa Utumishi wa Mamlaka ya Elimu Kibaha, Lucy Swai kujinyakulia bodaboda.
Washindi hao walifika kwenye ofisi za Global Publishers, Mwenge jijini Dar na kukabidhiwa zawadi zao zikiwemo bodaboda, Ving’amuzi vya TING na simu za kisasa (smartphone).
Lucy aliyeongozana na mumewe ambaye ni Kaimu Meneja wa Huduma za Tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi) iliyopo Kibaha, Dk. Mokiwa Athumani, alikabidhiwa bodaboda mpya aina ya Skymark Commuter.
Wakati wa kukabidhiwa zawadi zao, Afisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda alimkabidhi bodaboda yake, Lucy aliyekuwa pembeni ya mumewe karibu muda wote walikuwa na furaha.
Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Lucy aliushukuru uongozi wa Global na wafanyakazi wengine kwa kuandika habari motomoto zisizochosha na kufanikisha kushinda zawadi hiyo ambayo alisema itampunguzia tatizo la usafiri.
Lucy aliapa kutoiuza pikipiki hiyo bali atajifunza kuiendesha ili impunguzie kero ya usafiri hasa kuwawahisha watoto shuleni na kusisitiza kuwa ataendelea kucheza bahati nasibu hiyo mpaka anyakue zawadi ya nyumba inayotarajiwa kukabidhiwa kwa mshindi Juni, mwaka huu katika droo ya mwisho.
Mume wa Lucy ambaye alisema ni dereva wa gari, aliingilia kati maongezi hayo na kusema kuwa wakati mwingine atakuwa akiitumia pikipiki hiyo kumuwahisha kwenye safari zake.
“Unajua kuna wakati mwingine nakuwa na safari ambazo zinahitaji kuacha gari na kutumia bodaboda hivyo pikipiki hii imetatua suala hilo,” alisema Dk. Mokiwa.
Sambamba na Lucy kukabidhiwa pikipiki hiyo wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Francisca Kilalo wa Tandika, Dar aliyekabidhiwa vyombo vya jikoni, Agnes Pallangyo wa Singida (King’amuzi cha TING) ambacho kilipokelewa na baba yake David Nasali, Samwel Saitot wa Arusha ambaye ameshindwa kufika kwenye hafla hiyo atatumiwa King’amuzi cha TING mkoani Arusha.
Thomas Kilala wa Arusha naye alishindwa kuhudhuria hafla hiyo lakini aliwakilishwa na ndugu yake, Salim Mveyange ambaye alimchukulia zawadi yake ya King’amuzi cha TING.
Robert Wilson wa Dar naye alikabidhiwa King’amuzi cha TING, Lamla Musa wa Dar naye alishindwa kufika kwenye hafla hiyo aliwakilishwa na mwanaye Kassim Mbelwa aliyemchukulia zawadi yake ya King’amuzi cha TING.
Emmanuel Henry wa Dar alikabidhiwa simu ya kisasa na Halima Bashemela wa Igunga Tabora aliyeshindwa kufika atatumiwa zawadi yake ya shuka.
PICHA NA RICHARD BUKOS NA SALUM YASIN/GPL

No comments: