NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Bulyanhulu
KATIKA
kuadhimisha kilele cha siku ya Wanawake
Duniani leo Machi 8, 2016, akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu
wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia,huko wilayani Kahama mkoa wa
Shinyanga, wao walitembelea na kuona shughuli za uchimbaji madini chini ya
ardhi (Underground operations).
Akina
mama hao kutka kada mbalimbali za vikundi vya wajasiriamali, wakulima, na
viongozi wa dini, walifanya ziara ya kutembeela na kujionea shughuli za
uchimbaji madini chini ya ardhi kiasi cha kilomita 2 kutoka uso wa ardhi,
walieleza kufurahishwa kwao na kusema hata wao wanaweza.
Pamoja
na maeneo waliyoyatembelea, walijionea mashine za kuchironga miamba, pamoja na
karakana (gereji) ya kutengeneza magar na mashine zinazotumika kwenye eneo
hilo. Ziara hiyo iliwachukua takriban masaa matatu (3), na bila kuchoka
walikamilisha ziara hiyo na wote
walikuwa katika hali nzur nay a furaha.
Katika
tukio linguine, Mgodi huo ulimpatia kila mshiriki wa ziara hiyo, mche moja wa
matunda ili wakapande kwenye maeneo wanayoishi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya
mgodi kuhifadhi mazingira kwenye maeneo jirani na mgodi huo.
Siku
ya wanawake Duniani, huadimishwa Machi 8 ya kila mwaka ili kuelezea changamoto
mbalimbali zinazowakabili wanawake na kutafuta majawabu yake.
Mama huyu ambaye ni sister wa kanisa Katoliki, alikuwa miongoni mwa wanawake waliotembelea mgodi huo chini ya ardhi
Ramadhani Chura, (kulia), mchimbaji wa madini chini ya ardhi, akiwapa maelezo akina mama hao umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimsaidia mama huyu akuvaa kibuyu cha gesi ya oxygen kabla ya kushuka chini ya ardhi
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimuwekea kibuyu cha gesi ya Oxygen mama huyu tayari kaunza safari chini ya ardhi
Mkuu wa Uhusiano na mawasiliano wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Mary Lupamba, (kulia), akimsaidia mama huyu kuweka sawa kibuyu chake cha gsi ya Oxygen ili kutembelea eneo la uchimbaji chini ya ardhi
Hapa akina mama wako chini ya ardhi umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, wakipatiwa maelezo ya namna miamba inavyochorongwa kuipata dhahabu
"Wanawake tunaweza". ndivyo inavyoonekana kwa mama huyu akidandia gari la oeperesheni za chini ya ardhi kwenye mgodi wa Bulyanhulu wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo walipoadhimisha siku ya wanawake kwa kutembelea na kujionea kazi ya uchimbaji madini chini ya ardhi
Mwendesha mashine kubwa akiwa kwenye mashine yake
Mtaalamu wa kuchoronga miamba chini ya ardhi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, akiwapatia maelezo ya namna kazi hiyo inavyofanyika
Akina mama hao (kulia), wakiingia kwenye lango la kuelekea kupanda lifti ya kuwashusha chini ya ardhi
Hawa ndio akina mama shujaa waliomudu kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu chini ya ardhi kujionea kazi ya uchimbaji madini inavyofanywa, wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wanaohudumu kwenye eneo hilo
Mary akiwaongoza akina maam hao katika hatuaya awali ya kuelekea kwenye ziara ya chini ya ardhi
Fundi mitambo akiwa kwenye karakana (gereji) ya magari na mashine zinazofanya kazi kwenye eneo hilo
Akina mama shujaa wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment