Wednesday, March 9, 2016

MKUU WA MKOA WA MTWARA MH. HALIMA DENDEGU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2016 KATIKA UWANJA WA MASHUJAA.

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitoa Hotuba yake kwa wakazi wa Mtwara na Kuzindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la  OXFAM Tanzania
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Fatma Ally akizungumza na wakazi wa Mtwara,wageni mbalimbali na wadau pia kufungua rasmi sherehe hizo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani na Uzinduzi wa Shindano la Mama wa Chakula kwa Mwaka 2016
 Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Bi. Betty Mlaki akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika Hilo Jane Foster wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2016
 Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika kujenga Taifa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Sikukuu ya wanawake Duniani.
 Kamishna Msaidizi wa Polisi Tatu Abdallah Mfaume ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, akizungumzia juu ya Dawati la Jinsia linavyofanya kazi
 Mshereheshaji akiendelea na kutoa Utaratibu 
Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe za Siku  ya Mwanamke Duniani
 Bi. Jovitha Mlay Kutoka Shirika la Kimatafa la OXFAM Tanzania akizungumza na wakazi wa Mtwara juu ya wanawake na uziduaji
 Bw.  Mohammed Mapalala kutoka Morogoro anayehusika na Maswala ya Ardhi akizungumzia juu ya Haki ya Ardhi kwa wanawake
 Meneja wa Utetezi Kutoka Shirika la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akitoa Maelezo ya  kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo Msimu huu wa Tano linatarajiwa kuanzi mwezi Septemba na kurushwa katika Runinga ya ITV 
Mwanamuziki Vitaris Maembe akitoa Burudani ya Nguvu wakati wa Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitembelea katika Mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani a Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa Mwaka 2016
Mwanamuziki matata wa Miondoko ya Taarabu Jike la Simba Bi. Aisha Mashauzi akitoa Bonge la Burudani wakati wa kilele cha Siku ya wanawake Duniani
Burudani ikiendelea
Mamia ya wakazi wa Mtwara wakiwa katika Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2016, katika Uwanja wa Mashujaa.

Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la kimataifa la OXFAM  limezinduliwa rasmi  na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh Halima Dendegu na kuwataka washiriki kuuletea ushindi katika Mkoa wao wa Mtwara. 

Mh Halima Dendegu alitoa hamasa  hiyo katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akiwataka washiriki ambao ni wanawake wajitahidi kadiri wawezavyo mshindi wa shindano hilo atokee mkoani mtwara.

Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi za Umma, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mtwara pia Mh. Halima Dendegu alipata nafasi ya kugawa fomu za ushiriki kwa wakina mama watatu wa shindano hilo na kupata nafasi ya kuwaandikisha katika fomu hizo.

Pia katika hatua hiyo mkuu wa mkoa huyo amewaomba wakina mama wajasiriamali kujiokeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo ili kuongeza muamko wa shindano hilo na kujiongezea uwezo wa kushinda na kuwataka wanawake wajasiriamali kujaza fomu za ushiriki kwa wingi na bila ya kuogopa.

Sanjali na hatua hiyo mkuu wa mkoa amesema kuwa licha ya kuwepo na harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi ambao wengi wao wanaotegemea kilimo kama njia ya kujipatia mazao lakini bado kumekuwepo na changamoto kubwa kwa mwanamke ya kumiliki Ardhi ambapo ametaja kama moja ya changamoto ya ukandamizaji wa kijinsia na kuwataka wanawake kusimama kidete katika kutetea haki hiyo kama moja wapo ya msingi.

Naye Meneja wa Utetezi wa Shirika la Kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona alieleza kuwa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka huu 2016 linatarajiwa kuanza Septemba na litakuwa linaoneshwa kupitia kituo cha runinga cha ITV.

Meneja wa mradi kutokea shirika la OXFAM, Bi. Jovitha Mlay amewatoa hofu washiriki watakaoshiriki katika shindano hilo kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi na hasa ikiwa kama bahati kwa shindano hilo la Mama shujaa wa chakula kuzinduliwa mkoani mtwara na hivyo kuwataka wakina mama wajasiriamali wakubwa na wadogo kujitokeza kwa kuchukua fomu za ushiriki kwa wingi.

Aidha baadhi ya wanawake wadau wa OXFAM kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wametumia nafasi hiyo zaidi kwa kuwataka wajasiriamali wakina mama wa Mtwara kutumia fursa mbalimbali ili kuongeza kipato chao na kuacha suala la utegemezi kotoka kwa waume zao.
Uzinduzi wa Mama shujaa wa chakula ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali waliotoa burudani kwa wakazi waliofika katika uzinduzi wa shindano hilo; alikuwepo Valis Maembe, Mwasiti na Isha Mashauzi.

Shindano la mama shujaa wa chakula lililoanzishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam lililoanzishwa hapa nchini mnamo mwaka 2011 lenye lengo zaidi ya kumsaidia mwanamke kujitambua zaidi katika haki zake mbalimbali na kujitambua kama mwanamke na kumuinua kiuchumi.



No comments: