Thursday, March 10, 2016

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA AFYA BURE KUTOKA KWA BANGO SANGHO

Bango Sangho
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.
Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13 katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Akizungumzia huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa maendeleo ya taifa.
Alisema kupitia huduma hiyo madaktari watawapima watoto walio na umri chini ya miaka mitano afya ya kinywa, uzito, ukaguzi na ushauri wa lishe hivyo kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata huduma bure.
Ali Mzige
Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na waandishi wa habari.
“Tunataka kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.
Nae Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki Al Hilal alisema Bango Sangho kimekuwa chama ambacho kikisaidia jamii ya Tanzania katika sekta ya afya na wamekuwa wakitoa huduma ya kupima watoto bure walio na umri chini ya miaka mitano kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Alisema ripoti ya afya Tanzania inaonyesha kuwa kuna watoto 81 wamekuwa wakipoteza maisha kati ya watoto 1,000 walio na umri chini ya miaka mitano kutokana na sababu mbalimbali ambapo wamekuwa hawapati huduma na kupitia huduma hiyo ya kuwapima bure watoto walio na magonjwa wataweza kutambulika.
“Tutafanya huduma ya kupima bure watoto walio chini ya miaka mitano na tutakaobaini wanamatatizo maalum ya kiafya tutawapa rufaa ili wakapate huduma ya matibabu,” alisema Dkt. Mzige.
Huduma hiyo ya kupima watoto walio na umri chini ya miaka mitano ilifanyika pia mwaka jana na watoto 289 walipimwa afya zao huku baadhi walikutwa na matatizo ikiwemo maambukizi ya mfumo wa njia ya mkojo UTI, Utapiamlo, kukatwa vimeo na wengine wakionekana kuwa na afya duni.
Husna Abdallah
Mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Zawadi Chogongwe
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Zawadi Chogongwe (kulia) akiuliza swali kwa wataalamu wa afya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

No comments: