lilivyojipanga kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali ya ukuzaji wa elimu haapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali.
Alisema hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji elimu.
Alisema lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha watu wake kujiajiri.
Alisema kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha yao. Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe. Aidha amesema lengo la kushirikisha wadau wa elimu ni kuhakikisha kwamba lengo la maendeleo endelevu la nne la Umoja wa Mataifa linashirikishwa katika utoaji elimu kwani lengo hilo ni kuhakikisha elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi huku hatua zikichukuliwa katika kuwezesha wanawake kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment