Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya Upandaji MitiKimkoa . |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya
kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia
maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.
maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.
Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la
kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika
kilele cha upandaji miti kimkoa katika
eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.
Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na
kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa
mazingira katika maeneo yot.
"Nikazi
bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa
kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala.
Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda
miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo
vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya
kila siku.
"Serikali imeweka
lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo
lilipo fikiwa"Alisema
.
Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango
wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana
kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara
baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Mwisho
Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017 |
Afisa habari na Mawasiliano Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA)akichukua matukio katika tukio hilo la kilele cha upandaji miti kimkoa katika safu ya Mlima Mbeya Itagano. |
Mkutano ukiendelea......... |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti katika kilele cha Upandaji kimkoa katika chanzo cha Maji Hanzya Kata ya Itagano. |
No comments:
Post a Comment