Wednesday, January 11, 2017

MANDHARI TOFAUTI UNAZO KUTANA NAZO PINDI UNAPO PANDA MLIMA KILIMANJARO.

Uoto wa asili wa aina mbalimbali unavyoonekana wakati unapoanza safari ya kuelekea kituo cha Kibo ukitokea kituo cha Horombo.
Mawe yenye michoro mithili ya mistari ya Pundamilia yanaonekana katika eneo lijulikanalo kama Zebra Rocks.
Kwa mbali ni muonekano wa vibanda viwili maalumu kwa ajili ya kujisaidia ambavyo viko njiani wakati unaelekea Kibo Hut ,eneo hili linajulikana kama Last woter Point ni eneo la mwisho linaloonekana kuwa na maji.
Ndege wakubwa aina ya Kunguru mwenye baka jeupe shingoni
wanaonekana katika maeneo haya wakisubiri mabaki ya chakula kutoka kwa wageni wanaopanda Mlima Kilimanjaro.
Maeneo mengine yanaonekana kuwa na mabonde makubwa huku ukungu ukifunika uoto wa asili katika maeneo hayo.
Uoto wa asili hupotea kabisa na kubaki nyasi fupi hasa maeneo ambayo yamefunikwa na mchanga ,eneo hili ni maarufu kwa jina la Saddle .
Ukiwa njiani katika eneo hili unapata nafasi ya kupita katikati ya vilele viwili vya mlima Kilimanjaro yaani Kibo na Mawenzi na hiki ni kilele cha Kibo ilipo Uhuru Peak.
Hii ni sehemu tu ya vilima vilivyo njiani na eneo hili hutumika kwa ajili ya kupata chakula kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Kibo Hut.
Haya ni maeneo tofauti yanavyoonekana wakati wa safari ya kuelekea Kiboo Hut.
Ukipata bahati ya kuamka mapema ,hii ndio hali unayokutana nayo pindi uwapo katika safari ya kuelekea Kibo Hut.
Na huu ndio muonekano wa kituo kimojawapo majira ya asubuhi pindi kunapokuchwa.
Kwa mbaali taswira ya kilele cha Kibo ndivyo kinaonekana.
Upande wa pili kilele cha Mawenzi hivi ndivyo huonekana.
Njiwa pori pia wanaonekana katika maeneo haya.
Hii ni sehemu ya juu ya mlima ambayo hujulikana kama Jamaica ,sehemu ya mwisho kabla ya kufika Gilmans point.
Safari inayoendelea ni ya kupita eneo ambalo limezingirwa na barafu kuelekea kituo cha Stella.
Vilima vya barafu ni sehemu ya maumbile yanaoonekana katika eneo la jirani kabisa na kilele cha Uhuru.
Maeneo mengine licha ya kuwa juu ,yanaonekana kuwa makavu .
Na hapa ndio Kilele cha Uhuru ambako safari ya siku nne inakufikisha na kuandika historia kuwa miongoni mwa watu waliowahi kufika eneo la juu kabisa Afrika na la pili Duniani.

N Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

No comments: