Saturday, January 14, 2017

SERIKALI KUENDELEZA MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akimkabidhi zawadi Mkaguzi wa Polisi, David Mabula.
 Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki kutokana na ufanyakazi bora.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
 Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
 Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
 Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
 Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau 
kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari  wakiwa kwenye hafla hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kupambana wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

Mwigulu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Serikali imejipanga  kupambana na dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la kitaifa ambapo vijana wengi wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.

Mwigulu alisema serikali ya awamu ya tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye kwamisha jitihada za kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga kuupunguza kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2019.

Aliongeza kuwa kanuni na sheria zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani ya jeshi la polisi zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi. 

Akitolea mifano kadhaa alisema askari polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi hilo anapaswa kupewa fedha za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na suala hilo si la kumuonea huruma askari husika bali ni haki yake.

Alisema kwa upande wa askari polisi aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa mapambano dhidi yake na wahalifu askari huyo anapaswa kulipa fidia yake kwa wakati badala ya kuunda tume ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa katika mapambvano hayo.

"Mambo mengine hayahitaji mpaka uwe na elimu kubwa askari amepambana na majambazi mbele ya watu lakini majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake anashindwa kulipwa eti mpaka iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji Mwigulu.

Alisema kwa muda mrefu askari anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia kwa nauli na fedha za kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila ya sababu za msingi.

Alisema hali hiyo kama askari husika anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza katika tamaa na kutumia silaha aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba wahusika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwani mshahara na posho kwa askari hao ni haki yao.

Mwigulu alisema serikali kupitia Rais Dk. John Magufuli imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa askari polisi ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba na kuona namna ya kubadilisha sheria ambazo zinaonekana hazina tija kwa wakati huu katika kuliongoza jeshi hilo.

No comments: