Saturday, May 13, 2017

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, yagawia wateja wa Tigo Pesa faida ya jumla ya Sh 5.48bn/= kwa ajili ya robo ya pili ya mwaka 2017




Mkuu wa Kitengo cha Fedha-Tigo Pesa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Christopher Kimaro akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza gawio kwa robo ya pili ya mwaka 2017 ambapo jumla ya sh 5.48bn/= zimegawiwa kwa wateja wa Tigo Pesa. Kushoto kwake ni Mkuu wa kitengo cha Masoko Tigo Pesa, Catherine Rutenge.

 Dar es Salaam,  Mei 10,  2017- Watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa  wamelipwa  jumla ya 5.48bn/- kama faida ya  gawio  inayolipwa kila mwaka na kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tanzania.
 Hii ni mara ya 12 Tigo inagawa malipo ya robo mwaka  kwa watumiaji wa huduma ya fedha kwa simu tukio ambalo imekuwa ni kampuni  ya kwanza  ya simu kufanya hivyo duniani tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo Julai 2014.
 Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo inaonesha kuwa kampuni hiyo inalipa malipo hayo kwa  kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kilichoishia Machi 31, 2017
Kwa mujibu wa Mkuu Kitengo cha Fedha, Tigo Pesa Christopher Kimaro kwa ujumla watumiaji wa Tigo Pesa wameshapata 63.58bn/- kama faida ya gawio lao tangu kuanza kwa mpango huo ,mwaka 2014.   Malipo hayo ni faida inayotoka katika akaunti za Mfuko wa Tigo Pesa ambazo zimo katika mabenki makubwa ya biashara nchini.
 Wanaopokea gawio hilo ni pamoja na wateja binafsi, mawakala wa rejareja, mawakala wakubwa na washirika wengine wa kibiashara wa Tigo Pesa ambao kila mmoja anapokea malipo hayo kulingana na kiasi cha thamani ya fedha-elektroniki waliyonayo kila siku  ndani ya pochi zao za Tigo Pesa,” alisema Kimaro katika taarifa hiyo.
 “Tunayo furaha kutangaza gawio hili la faida  kwa mara ya 12 mfululizo. Hili liko katika mikakati yetu ya kujikita kutoa  na kufikiwa kwa huduma za kifedha kwa wateja wetu na nchi kwa jumla  kupitia huduma zetu za Tigo Pesa,” alisema Kimaro.
Alibainisha kuwa kuongezeka kwa faida katika Tigo kunaboresha mazingira ya soko na kukua kuliko imara kwa idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa. Tigo Pesa hivi sasa  ina mtandao mkubwa wa wafanya biashara zaidi ya 80,000 kote nnchini.
 “Tigo ni kampuni ambayo bado inakua kwa kasi ikiwa ni kama motisha kwa uaminifu wa chapa Tigo  iliyoamua mwaka 2014  kuwazawadia wateja wake kupitia faida ya gawio, na wakati huo huo ikiwekeza kwa kadri inavyoweza  katika kukua zaidi,”alisema Kimaro.
Kama ilivyokuwa awali gawio hilo kwa wateja kwa mujibu wa Kimaro linakokotolewa  kulingana na wastani wa kila siku wa fedha za mteja zilizomo katika  pochi yake ya simu ya Tigo Pesa na kwamba kugawanywa kwa gawio  hilo la faida  upo katika Waraka wa Benki Kuu uliotolewa Februari 2014.

 Mwisho

No comments: