Tuesday, May 9, 2017

MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA NA UVUVI HARAMU YASHIKA KASI WILAYANI NYAMAGANA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe.Marry Tesha (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mapambano ya dawa za kulevya, uvuvi haramu na makosa mengineyo wilayani humo.
#BMGHabari
Mkuu wa polisi wilayani Kamagana akizungumza kwenye kikao hicho
.
Katibu wa mkuu wa wilaya ya Nyamagana akizungumza kwenye kikao hicho
Afisa uvuvi halmashauri ya Jiji la Mwanza akizungumza kwenye kikao hicho
Wakili wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Mwanza, akizungumza kwenye kikao hicho.
Wakili wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Mwanza, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana (kulia), wakiwa kwenye kikao hicho
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe.Marry Tesha, amesikitishwa na taarifa za utekelezaji wa mapambano ya dawa za kulevya, uvuvi haramu na makosa mbalimbali ya kiusalama wilayani humo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Akizungumza ijumaa iliyopita kwenye kikao hicho mwishoni mwa wiki, Mhe.Tesha, alisema taarifa zilizowasilishwa na baadhi ya watendaji hazikuwa zimejitosheleza na kuwataka watendaji hao kuhakikisha kikao cha mwezi ujao wanaandaa taarifa kamili ikiwemo mafanikio na mapungufu halisi katika mapambano hayo. 

Kikao hicho kiliwahusisha viongozi kutoka idara mbalimbali ikiwemo polisi, uvuvi, serikali za mitaa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambapo taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, OCD Ochieng Asiago, ilibainisha kukamatwa kwa watuhumiwa 15 na kesi 16 kutokana na dawa za kulevya.

Awali baadhi ya wajumbe katika kikao hicho waliwatupia lawama maofisa wa serikali kwa kuharibu ushahidi wa dawa za kulevya ikiwemo kuita kokeini kwamba ni unga sembe.

Hata hivyo Wakili wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Mwanza, Seth Mkemwa, alifafanua kwamba dawa zinazohisiwa ni za kulevya zinapokamatwa lazima zifikishwe ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi na ikibainika ni dawa halisi watuhumiwa kufikishwa mahakamani na dawa kuteketezwa.

No comments: