Usimamizi usiofaa wa miradi mbalimbali ya maji nchini umeelezwa
kuwa ni kikwazo kwa juhudi za kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kila familia.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Injinia Jackson Mutazamba katika semina ya inayofanyika mjini Morogoro
ikijuimuisha wakurugenzi kutoka halmashauri zote nchini.
Alisema lengo la semina hiyo ni kuweza kuwahimiza na kuwajengea
uelewa zaidi wakurugenzi hawa namna ya kufanya miradi ya maji iweze kuwa na
tija na kufanya upatikanaji wa maji kwa wananchi isiwe kikwazo.
"Utawala bora katika usimamizi wa miradi ya maji ni kitu cha
msingi sana katika kufanya miradi ya maji iwe endelevu mara baada ya kuanzishwa
na kuweza kuwapatia wananchi maji wakati wote wa mwaka," alisema.
Alisema hadi mwezi wa tatu mwaka huu mtandao wa maji ulikuwa
umefikia asilimia 72 nchini pote lakini miradi mingine haifanyi kazi kutokana
na utawala mbovu hivyo kufanya kuwe na upungufu mkubwa wa maji.
Alisema wakurugenzi wa wilaya ni viungo muhimu sana katika kufanya
miradi hii ya maji iwe endelevu ukizingatia kuwa serikali na wadau wa maendeleo
wamekuwa karibu sana katika kuhakikisha miradi mingi ya maji inaanzishwa.
Pia wakurugenzi wanaweza kusimamia uanzishwaji wa kamati maalumu
za maji ambazo zinasimamiwa moja kwa moja na wananchi wenyewe hivyo kufanya
miradi hii iwe endelevu.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka 2017/18 bungeni Dodoma
wiki iliyopita, Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwenge
alisema serikali imejipanga kuanzisha miradi mipya mingi ili kuweza kuongeza
mtandao wa maji kufikia asilimia 95.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mpanda Rojas John Lomuli akiahidi
kuitikia wito wa kuendeleza usafi wa mazingira ili kuhakikisha halamashauri
yake
inafikia kiwango cha juu katika utekelezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro
inafikia kiwango cha juu katika utekelezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro
Mkurugenzi wa
halmashauri ya kondoa Khalifa Kondo akionyesha ishara ya kampeni ya Nipo Tayari ya kutekeleza usafi wa
mazingira katika mji wake wakati wa semina ya kwa wakurungenzi wa halamashauri
nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi mkoani
Singida Rustika Turuka akielezea matarajio yake wakati wa semina ya utekerezaji
wa kampeni ya Nipo Tayari
iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa
matokeo, inayofanyika mjini Morogoro
No comments:
Post a Comment