Bi.Esther Masomhe, akizungumzia mikakati ya Manispaa yake kuhusu mazingira na utunzaji wake
Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya
Kilimanjaro Dialogue Institute, (KDI), Bw. Habib Miradji
Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Bw. Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.
Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Bw.Hassan Mzighani,
(kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi
Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na
mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini
sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.
NA KVIS BLOG/Khalfan Said
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora.
Akizungumza kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo, Bi.Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji, (City beatification).
“Kuna maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff, barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge, tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.
Akifafanua zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake.
Aidha Afisa huyo wa Mazingira wa wilaya ya Ilala alisema, kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ““Hifadhi Mazingira, kama Muhimili wa Maendeleo ya Viwanda”
“kauli mbiu hii ina maana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimejengwa bila kuzingatia uhifadhi wa mazingira, utakuta mtu mwenye kiwanda, anashindwa kuhifadhi maji taka anayozalisha na badala yake anatiririsha kwenye mito, ambako huko kuna viumbe hai, sihilo tu lakini pia kuna watu wanaendesha kilimo cha mboga mboga, kwa vile maji wanayotumia ni hayo hayo ya mto ambayo tayari yanakuwa yamechanganyika na maji taka ya viwandani, walima bustani hutumia maji hayo kunyweshea bustani zao na hivyo kuwalisha wananchi mboga mboga zenye kemikali, nah ii ni hatari kwa afya,” alisema
Alisema kwakuwa sheria zipo wazi, watasimamia sheriahizo kikamilifu ili kuhakkiikisha kiwanda kitakachoanzishwa kwenye Manispaa knazingatia uhifadhi wa mazingira.
Naye Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Habib Miradji amesema, “hakuna mtu ambaye hafahamu umuhimu wa mazingira, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la kimazingira, sisi tunaetembea dunia tunaona kuna milima misitu ya asili na mbuga, kwa kweli inabidi ukae ufikirie jinsi maliasili ilivyotunzwa, lakini hapa kwetu, vitu kama hivi havipo, ilikuwa zamani tu maana hata milio ya ndege na miti asili imetoweka.” Alisema.
Bw. Miradji alihoji nini mikakati ya Manispaa katika uhifadhi wa mazingira kwani maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hususan uswahilini, (urban slams) haya yanakuwa na ongezeko la watu kwa haraka, familia moja inawezakuwa na watu 10 na zaidi, nini mkakati ya Manispaa katika kukabiliana na misongamano ya watu?
Akijibu hoja hiyo Bi. Masomhe alsiema, kumekuwepo na mikakati mbalimbali ikiwemo ya utoaji elimu mashuleni, kupitia klabu za mazingira za shule, lakini pia kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kupitia kwa maafisa afya wa Manispaa ambao hutembelea mara kwa mara ili kutoa elimu ya usafi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment