Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa,(wapili kulia), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martn, akifungua semina hiyo leo Juni
8, 2017
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
ZAIDI
ya wawakilishi 250 wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kutoka jijini Dar es
Salaam wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wake wa
uchangiaji wa hiari (PSS), baada ya kushiriki semina ya siku moja makao makuu
ya Mfuko jijini Dar es Salaam Juni 8, 2017.
Wanafunzi
hao kutoka taasisi 20 za elimu ya juu, wamehudhuria semina hiyo ya siku moja
iliyoandaliwa na PSPF kwa uratibu wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO),
ili kuwapatia elimu wanafunzi hao kuhusu shughuli za Mfuo na faida azipatazo
mwanachama ikiwemo mafao mbalimbali.
Kabla
ya zoezi hilo la kujiunga na Mfuko, awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi.
Costantina Martin, aliwaasa wanafunzi hao kujijengea utamaduni wa kuweka akiba
kwani manufaa yake huonekana katika kipindi kifupi.
“Mimi
nina mototo yuko chuo kikuu huwa ninampatia fedha kidogo za kujikimu lakini
namueleza aweke akiba, ningependa kuwahamasisha vijana mjenge utamaduni wa kujiwekea
akiba kidogo kidogo,zile posho mnazopata, na fedha kutoka kwa wazazi wenu,
mnaweza kutenga sehemu ya fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ili
kujiwekea akiba.” Alsoema Bi. Costantina Martin, wakati akifungua semina hiyo.
Alisema,
PSPF, kama Mfuko wa hifadhi ya jamii, moja ya malengo yake ni kuandikisha
wanachama wapya , kukusanya michango, kuwekeza na kuwalipa mafao na pensheni
wastaafu na wategemezi iliw aweze kupata fedha kwa ajili ya matumizi yao ya
kila siku.
Aliwashauri
wanafunzi hao kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, ili hatimaye waanze
kufaidi mafao mbalimbali ikiwemo faola matibabu ambapo mwanachama anapatiwa
bima ya afya itakayomuwezesha kutibiwa yeye mwanachama na wategemezi wake.
Ili
kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama, PSPF inaendesha mipango ya aina
mbalimbali ya uchangiaji, mpango wa lazima na mpango wa hiari ili kuhakikisha
kila Mtanzania anakuwa salama katika Hifadhi ya PSPF.
“Najua
wataalamu wetu watawapa elimu ya kutosha kuhusu aina za wanachama kwani hata
ninyi mnaweza kuwa wanachama wetu kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari PSS,
ambapo mnaweza kujiunga na kupatiwa kadi zenu leo hii baada ya semina.”
Alsiema.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO),
Bw.Stanslaus Peter Kadugalize, ameishukuru PSPF kwa kuwa mshirika mzuri na
kukubali ombi la wanafunzi hao kupatiwa elimu juu ya hifadhi wa jamii.
“
Ninachoomba, PSPF inaweza kuangalia namna gani inaweza kusaidia wanafunzi
katika ushiriki wao kwenye elimu, kwa mfano mnaweza kutusaidia hata kutujengea vimbweta
kwenye vyuo vyetu, lakini pia mnaweza,uwekeza kwenye ujenzi wa hosteli ambazo
sisi wanafunzi tutalipa kodi.” Alsiema.
Maafisa
wa PSPF, walitoa mada mbalimbali ambazo miongoni mwake ni pamoja na jenga
career na PSPF, ambao ni mkopo wa elimu, Jipange kimaisha na PSPF, ambapo PSPF
hutoa mikopo kwa mwajiriwa mpya,
Hata
hivyo wanafunzi hao waliiomba PSPF kutengeneza mfumo ambao unaweza kuwasaidia
wanafunzi kuwawezesha nkushiriki kwenye elimu bila matatizo. “Wanafunzi
hawahitaji fedha nyingi, mnaweza kuweka mfumo utakaowawezesha wanafunzi kupata
mikopo midogo ya fedha ili kuwawezesha kujikimu wawapo vyuoni na hatimaye
wanafunzi hao wanaweza kurejesha fedha hizo kwa utaratibu utakaokubaliwa na pande
mbili.
Mwenyekiti wa TAHILISO, Bw.Stanslaus Peter Kadugalize,(aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo mwishoni mwa semina hiyo. Wengine kutoka kushoto, ni Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi. Zuhura A. Rashid, Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi.Zuhura A.Rashid, (kushoto), akijaza fomu ya kujiunga na PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
Viongozi wa wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na PSPF
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi.Costantina Martin,akifungua semina hiyo
Kely Malinga, wa call centre ya PSPF akiwa kazini
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, akizungumza kwenye senima hiyo
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, akizungumza kwenye senima hiyo
Afisa Matekelezo wa PSPF, Bw. David Mutabazi, akitoa mada yake jinsi masuala ya hesabu za kulipa mafao zinavyofanyika
Bi. Neema na Bw. Njaidi wakiwaongoza washiriki wa semina hiyo, kutembelea pfisi za PSPF ili kujionea utendaji kazi wa ofisi hizo kabla ya kuanza semina
Washiriki wakijisajili
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akizunguzma na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu, walipotembelea kuona jinsi utunzaji taarifa za wanachama wa Mfuko zinavyohifadhiwa. Hii ilikuwa ni sehemu ya semina waliyopewa viongozi hao na maafsia wa PSPF jijini Juni 8, 2017
Washiriki wakionyeshana fomu za PSS, za wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari
Afisa wa PSPF anayeshughulikia masoko, Bw. Magira Werema akizungumza wakati wa kutoa elimu viongozi hao wa wanafunzi
Afisa wa PSPF anayeshughulikia masoko, Bw. Magira Werema akizungumza wakati wa kutoa elimu viongozi hao wa wanafunzi
Mshiriki akijaza fomu za kujiunga na PSS
Washiriki wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha za vitambulisho vya kadi za uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS
Afisa mwandamzi wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Bw. Delphis Richard, (kushoto), akitoa mada iliyoelezea faida
mbalimbali azipatazo mwanachama wa Mfuko huo kwa washiriki
Washiriki wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
Bi. Neema(kushoto), akimuelekeza jambo mshiriki huyu wa semina
Mkuu wa idara ya call centre, Bi Queen, (katikati), akitoa maelezo kwa washiriki walipotembelea ofisi za huduma kwa wateja, za PSPF makao makuu
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Costantina Martin, (katikati), akiongozana na Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa
Pensehni wa PSPF, Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Lowassa, (kulia) na Afisa
Mwandamizi wa Utafiti, Mapesi Maagi. Kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano ambako
kulifanyika semina ya siki moja ya viongozi wa serikali za wanafunzi wa elimu
ya juu jijini Dar es Salaam jana Juni 8, 2017.
Afisa mwandamizi wa kitengo cha utunzaji kumbukumbu (record keeping), Bw. Gwamaka A. Ngomale, (mwenye kofia), akiwaeleza washiriki hao namna PSPF inavyotunza kumbukumbu kwenye mfumo wa kielektroniki wa makabati (electronic shelves)
Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi.Zuhura A. Rashid, akitoa neno la shukurani baada ya semina kumalizika
No comments:
Post a Comment