H
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa
uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema
Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
NA K-VIS BLOG, DODOMA
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani
Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu.
Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu.
Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa
wastaafu watarajiwa mkoani Dodoma Julai
14, 2017.
Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili
kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma
utakapokoma.
Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka
michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero
kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana
na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kutokamilika.
“Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika
kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni
vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya
kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na
ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi
wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.
Katika hatua nyingine, wimbi la viongozi kujiunga na Mpango wa
uchangiaji wa Hiari yaani PSPF Supplementary
Scheme, (PSS), Mhe. Jafo naye amejiunga na mpango huo na kuwahamasisha
wastaafu hao watarajiwa na wananchi wengine kujiunga na Mpango huo kwani
utawawezesha kuwa na hakikisho la kuweka fedha zao ili ziwasaidie kwenye miradi
wanayotarajia kuibuni, ikiwa ni pamoja na kujipatia bima ya afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu,
amebainisha kuwa mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika
kipindi cha 2017/18 ambazo ni Mafao ya watumishi 9,552 wanaojiandaa kustaafu
katika kipindi cha kati ya Mwaka huu wa 2017 na mwaka ujao wa 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Mzee mstaafu akitoa ushuhuda kwa kundi la wanachama wa Mfuko wa
PSPF wanaotarajiwa kustaafu katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani
Dodoma.
No comments:
Post a Comment