Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
SHAHIDI wa
utetezi katika kesi ya kughushi Mukhtasari,wa serikali ya mtaa wa Levolosi ,mfanyabiashara
,Mathew Moleli ameieleza mahakama jinsi mkuu wa wilaya mstaafu alivyoingia kwa mabavu nyumbani kwake na
kuamrisha askari polisi aliokuwa ameambatana nao wapekuwe chumba chake
wakitafuta hati inayodaiwa kughushiwa.
Akitoa
utetezi mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga
wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ,anayesikiliza shauri hilo huku akiongozwa
na wakili wa utetezi Ephraim Koisenge, aliieleza mahakama hiyo jinsi
alivyofedheheshwa wakati askari hao,akiwemo mwendesha bodaboda na mlalamikaji
Makanga walivyopekuwa chumba chake wakitafuta hati ambayo ni mali.
Shahidi huyo
aliiendelea kueleza kuwa, mnamo oktoba ,2 mwaka 2014 alishtakiwa katika
mahakama ya wilaya iliyopo Sekei mkoani Arusha, kwa shauri kama hilo huku
mlalamikaji akiwa ni Danny Makanga na baadae oktoba 1,mwaka 2015 kesi hiyo
ilifutwa baada ya upande wa jamhuri kuomba kuondoa shauri hilo mahakamani jambo ambalo anadai linampotezea muda wake.
Alidai kuwa kufutwa kwa shauri hilo aliandika
barua kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa ARUSHA (RCO) kuomba kurejeshewa hati yake ya nyumba iliyokuwa inashikiliwa
ofisi ya RCO, jambo ambalo hakuwahi kujibiwa hadi oktoba ,28 mwaka 2016
alipokamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani
akishtakiwa kwa makosa mawili ya
kughushi Mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kuwasilisha nyaraka za
kughushi katika ofisi za jiji la Arusha ,
Hata hiyo
upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mary Lucas ulimtaka
mshtakiwa kueleza uhalali wa eneo anakoishi kwa sasa ,jambo ambalo shahidi huyo
alisema ni mali yake na waliuziana kindugu na mlalamikaji Makanga bila kuandikishana na baadae alifuata taratibu
zote za kuomba hati miliki kupitika kikao cha dharura kwa uongozi wa serikali
ya mtaa wa Levolosi kilichoketi Septemba,10 mwaka 2006.
Pia shahidi
huyo alieleza kuwa tangu kikao hicho cha serikali ya mtaa kiketi kwa dharura na
baadae kupeleke maombi ya kupatiwa hati ya umiliki wa nyumba yake kiwanja namba
231 kitalu DD kilichopo Mianziani jijini Arusha ,hakuwahi kupata malalamiko
yoyote kuhusu kughushi nyaraka za serikali,jambo ambalo ameiomba mahakama
kuifuta kesi hiyo kwa sababu malalamiko hayo hayana ukweli wowote.
Kesi hiyo
namba 430 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuendelea tena ,Septemba 28 mwaka huu
,ambapo upande wa utetezi unatarajia kufunga utetezi wake kwa shahidi wa pili
na wa mwisho baada yashahidi wa kwanza ambaye ni mshtakiwa kukamilisha utetezi,ambaye
pia aliwasilisha nyaraka mbalimbali kama
vielelezo mahakamani hapo.
Awali wakili
wa serikali Mary Lucasi alipinga kuwasilishwa kwa baadhi ya nyaraka muhimu za
mshtakiwa mahakamani hapo kwa madai kuwa nyaraka hiyo ni kivuli ,jambo ambalo lilipigwa na
wakili wa utetezi Koisenge ambaye aliiomba mahakama izipokee kama kilelezo,jambo
ambalo hakimu Mwankuga baada ya kuzipitia hoja ya upande wa mashtaka aliona
hazina mashiko na kuzipokea ili zitumikea mahakamani hapo kama kielelezo.
No comments:
Post a Comment