Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza
wakati wa ufungua wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua
wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Nobert Kahyoza
akiwasilisha hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA wakati wa mkutano wa wadau na
watumiaji wa huduma ya maji Manyoni. Wengine ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses
Matonya akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa huduma ya maji
kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo ambaye ni Mhe Mtaturu.
Meneja Ufundi wa Mamlaka na Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa
Manyoni (MAUWA) Ndg Maduhu Shija akiwasilisha taarifa ya mapitio juu ya maombi
ya kubadili bei za maji.
Baadhi ya wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira wakifatilia Mkutano. Mkazi wa eneo la Manyoni Mjini ambaye ni mdau wa huduma ya mamlaka ya Maji Bi Bahati Suleiman Matonya akichangiamada wakati wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya wakati wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.
Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
leo Octoba 20, 2017 amefungua Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira juu ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya maombi
ya Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Wilaya ya Manyoni (WSSA) ya
kurekebisha bei za Huduma za Maji Safi.
Akizungumza Wakati wa ufunguaji wa
Mkutano huo ulioandaliwa na (EWURA) na kufanyika katika Ukumbi wa Maktaba Mhe
Mtaturu Alisema kuwa Maji Ni Huduma muhimu kwa wananchi na uchumi wa Nchi
yoyote ile na upatikanaji wake Ni kielelezo tosha Cha ubora wa maisha ya watu
wote kwa ujumla hivyo Mkutano huo Ni dira ya maboresho ya upatikanaji maji kwa
ajili ya kuwapunguzia kadhia wanayokumbana nayo wananchi ikiwemo umbali kwa
ajili ya kuifikia Huduma hiyo.
Alisema kuwa Mwaka 2001 Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya kuanzisha chombo chenye
jukumu la kudhibiti na kusimamia watoa Huduma (EWURA) katika sekta ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira ikiwa Ni pamoja na sekta ya nishati ambapo baadhi ya
majukumu yake Ni pamoja na kudhibiti ubora wa Huduma ya Maji nchini kwani awali
Huduma za Maji zilikuwa zikisimamiwa na serikali kupitia Wizara ya Maji kwa
kutumia Sheria na mikataba mbalimbali.
Alisema Uundwaji wa Mamlaka za
udhibiti Kama EWURA Ni kielelezo Cha utekelezaji wa kanuni za utawala Bora
wenye lengo la kutenganisha majukumu ya kuandaa sera na kusimamia utekelezaji
wake kwa upande mmoja, na yule wa udhibiti kwa upande mwingine ambapo serikali
imebaki na jukumu la kuandaa sera na kuwasilisha miswada ya Sheria Bungeni,
Kusimamia utekelezaji wa sera na mikakati yake, Kuwezesha wananchi kushiriki
katika masuala yanayohusu mustakabali wao na kuhamasisha wawekezaji kushiriki
katika maendeleo ya sekta na KUJENGA miundombinu.
Mhe Mtaturu Alisema kuwa pamoja na
Mkutano huo wa majadiliano Kati ya wadau wa maji Wilayani Manyoni lakini
wananchi wanapaswa kutambua kuwa ili kuboresha Huduma za upatikanaji wa maji
pia Ni muhimu wananchi kutunza Mazingira kwani maji Yana mahusiano ya Moja kwa
Moja na Mazingira.
Mhe Mtaturu Alisema kuwa uharibifu
wa Mazingira Ni chanzo Cha upatikanaji hafifu wa maji hivyo wanachi wanapaswa
kupanda miti kwa wingi ikiwa Ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji.
Sambamba na hayo pia aliitaka
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa Manyoni (MAUWA)
Inayojihusisha na Huduma ya usambazaji maji Safi na salama ndani ya Mji wa
Manyoni kutoa taarifa sahihi ya utendaji kazi kwa wateja wao na EWURA lakini
zaidi kusimamia kwa umakini jukumu lao la Msingi la utoaji Huduma na bidhaa
Bora na kwa Wakati kwa watumiaji wengi zaidi.
Mhe Mtaturu alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kujenga uwezo wa kupata fedha za kuimarisha miundombinu ya kusambaza maji ili kutimiza dhamira ya kuwawezesha wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.
Awali akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Nobert Kahyoza ambaye ni Meneja wa EWURA
Kanda ya Kati Alisema kuwa Bei ya ada zinazotozwa Sasa na Mamlaka ya Maji
Manyoni kwa ajili ya Huduma zake zilipitishwa mwaka 2011 hivyo ili kuongeza
ufanisi katika Huduma ya utoaji maji EWURA imeamua kujadiliana na wadau wake
ili kurekebisha gharama za Maji.
Marekebisho hayo ya Bei yatayahusu
makundi yote ya wateja kwani marekebisho hayo ya Bei yatasaidia kupata fedha za
kutosha kukidhi gharama za uendeshaji Kama vile uzalishaji na matengenezo vya
vipuri mbalimbali.
Naye Meneja Ufundi wa Mamlaka na
Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa Manyoni (MAUWA) Ndg Maduhu Shija Alisema kuwa
uzalishaji wa maji kwa ajili ya Mamlaka ya Maji Manyoni unafanyika katika
maeneo ya Mitoo Mbugani (Visima 8), Kaloleni kisima Kimoja, Na Mitoo ya Chini
Kisima kimoja ambapo kea ujumla Visima hivyo vina uwezo wa kutoa lita 794,000
kwa siku.
Alisema miongoni mwa mikakati ya
utatuzi Ni pamoja na kuongeza vyanzo vya maji kwa kuchimba Visima Vinne ndani
ya miaka mitatu ijayo, na Kuongeza idadi ya wananchi wanaopata Huduma ya Maji
Safi na salama kwa kuongeza idadi ya maunganisho ya maji katika makundi yote na
kupeleka mtandao wa maji kwenye maeneo ya Jasiliamali, Kaloleni ya Chini,
Mwembeni, Chang'ombe na Mitoo ya Chini.
Mikakati mingine Ni kuendelea kuomba
fedha kwa ajili ya utekelezaji mkubwa wa Mradi wa maji wa Tsh Bilioni 19 kwa
ajili ya kuboresha Huduma ya maji, Kununua madawa ya kutibu maji
yatakayowezesha maji yanayosambazwa kwa wateja na kupendekeza marekebisho ya
Bei za Maji.
AIDHA, Katika Mkutano huo Wadau na watumiaji wa maji, Baraza la ushauri la watumishi wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), Baraza la wawakilishi la serikali (GCC) wamepinga vikali ongezeko la zaidi ya asilimia 100% kwenye gharama za upatikanaji wa huduma za maji safi na Usafi wa Mazingira Manyoni.
MWISHO
No comments:
Post a Comment