Tuesday, November 14, 2017

TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)


 Meneja Mwandamizi  wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya,
(wapili kushoto), na wafanyakazi wenzake, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, kwa Mkurugenzi Myendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Muhammed Janabi, (mwenye miwani), katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 14, 2017. Msaada huo w afedha utawezesha matibabu ya moyo kwa watoto watano waliolazwa kwenye taasisi hiyo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa msada wa Shilingi milioni 10 kusaidia matibabu ya watoto wanaougua maradhi ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2017.
Akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya alisema, baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Taasisi hiyo inahitaji msaada ili iweze kuwafanyia upasuaji watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo, uongozi wa TANESCO ulisikia maombi hayo.
Kwa kawaida upasuaji kwa motto hugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 2.
“Tumekuwa na uhusiano mzuri na Taasisi yako, kwa hivyo japo hatuna uwezo mkubwa lakini Mkurugenzi Mtendaji aliona ni vema tutoe msaada wa kuwezesha upasuaji wa watoto watano, na leo tutakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10.” Alisema Mhandisi Mgaya katika hafla ya kukabidhi hundi hiuyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JKCI, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Aidha Mhandisi Mgaya alisema mbali na msada huo wa fedha, TANESCO pia imeondoa tatizo la upatikanaji wa umeme wa kutosha kwenye taasisi nhuyo kwa kuwawekea huduma maalum ili kuhakikisha umeme unapatikana bila ya shida yoyote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakayab Kikwete, Profesa Mohammed Janabi, alisema ili kuenzi msada huo wa TANESCO, mmoja wa watoto watakaofaidika na msada huo atapewa jina la TANESCO.
“Tutawaalika katika hatua ya mwamzo kabla ya upasuaji ili muone hali halisi ya mgonjwa na baada ya upasuaji na tutamuita TANESCO motto huyo.” Alisema Profesa Janabi wakati akitoa shukrani zake.
Naye Daktari bingwa wa moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani alisema kwa mwaka Taasisi hupokea wagojwa wanaohitaji upasuaji kiasi cha 200,000, kwa hivyo msada huo na minbgine kutoka kwa wasamaria husaidia pakubwa katika kuokoa maisha ya watoto wa Kitanzania.
“Tunawashukuru sana kwa msada wenu na tunaomba muendelee kusaidia jamii katika kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatriwa matibabu ya moyo hata kama uwezo wao ni mdogo.” Alisema Dkt. Majani.
Katika hatua nyingine wafanyakazi wa TANESCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa kwenye taasisi hiyo wanaosubiri kufanyiowa upasuaji.

 Mhandisi Mgaya na Profesa Janabi, wakimsikilzia Mwenyekiti wa TUICO, Tanesco, Bw.Hassan J.M Athumani, wakati akitoa shukrani.
 Profesa Janabi (kulia), akimkabidhi jarida la taasisi hiyo, Mhandisi Mgaya
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia), akisalimiana na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani.
 Bi. Muhaji akikabidhi msada wa maji, na mahitaji mengine, kwa muuguzi wa zamu wa wodi ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, Bi.Joyce Mtanga
 Mwenyekiti wa TUICO Tanesco, Bw. Hassan J.M Athjumani, (kulia), akikabidhi maji kwa mzazi wa mtoto aliyelazwa JKCI akisubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.





Mtoto MrishoHaidari(Miezi 7), ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo akiwa wodini akisubiri kufanhyiwa upasuaji.

No comments: