Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa hiyo kuashiria uzinduzi wa bidhaa za Sugar Free uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga akikabidhiwa zawadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akipatiwa zawadi.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
Uzinduzi huo.
Makofi yakipigwa katika uzinduzi huo.
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.
Meza kuu ikifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mada zikitolewa kuhusu bidhaa hizo.
Maelezo kuhusu bidhaa hizo yakitolewa.
Majadiliano yakifanyika.
Taswira ya ukumbi wakati wa uzinduzi huo.
Ukumbi ulivyokuwa.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Abacus Pharma (A) LTD imezindua bidhaa za Sugar Free ambazo zitatumika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wa kisukari nchini kutokana na bidhaa hizo kutokuwa na sukari wakati wa matumizi yake.
Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Best Western, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula.
Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.
"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.
Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.
Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Akizungumza katika uzinduzi huo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.
Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika.
Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.
Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.
Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.
Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.
No comments:
Post a Comment