Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland.
Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao
Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Muonekano wa chumba cha mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
MAONYESHO ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi mbili mwezi huo.
"Wanafunzi wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.
Kamugisha alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.
Alisema onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)
"Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Alisema udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kamugusha aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.
No comments:
Post a Comment