Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine
Shigella akizungumza na Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia wakati alipomtembelea ofisini
kwake kufanya
mazungumzo naye pia alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe kushoto ni
mazungumzo naye pia alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe kushoto ni
Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho
Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili kutoka kulia akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia kitu wakati
walipotembelea kituo hicho
Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia mitambo iliyopo
kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga
wakati
walipotembelea kituo hicho kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya
Korogwe,Rehema Bwasi
Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakitembelea mitambo iliyopo
kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga
wakati
walipotembelea kituo hicho
Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Meneja wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kulia ni Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia
Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme kutoka Tanesco Makao Makuu Bakaya Mtamakaya akizungumza wakati ziara hiyo ya Balozi wa Sweden
nchini Tanzania Katarina Rangnitt kushoto kulia ni Meneja wa Uzalishaji wa Kituo cha Pangani Hydro Systems
Meneja Uzalishaji wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kushoto akiteta jambo na na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt kushoto |
Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho. |
SERIKALI ya Sweden imetoa kiasi
cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na dola za
Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika
Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani
Tanga.
Hayo yamebainishwa na Balozi wa
Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo
ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Amesema
kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa
kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.
Amesema
kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona
umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho
cha fedha katika kukarabati mgodi huo.
"
Nishati ni jambo muhimu katika maendeleo ya viwanda na Tanzania tayari
imeweka mikakati mizuri katika maendeleo ya viwanda hivyo,serikali ya
Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha kwa kukarabati mgodi huo "alisema.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amemshukuru balozi
huyo kwa serikali ya Sweden kufadhili mradi huo,pia amemkaribisha balozi
huyo kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na uchumi.
"
Nawashukuru serikali ya Sweden kwa kufadhili mradi huo na mheshimwa
Rais ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji mkoani Tanga haswa katika
sekta ya viwanda hivyo karibuni Tanga mje kuwekeza" alisema.
Kwa
upande wake Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Hale Mhandisi
Steven Mahemba amesema kuwa mtambo huo umepunguza uzalishaji kutokana na
changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa mitambo.
"
Kituo hiki kimejengwa kuanzia mwaka 1962 na kumalizika mwaka 1964 na
kina muda wa takribani miaka 52 hivyo pia kutokana na uchakavu wa
miundombinu take imepunguza uzalishaji kutoka megawati 21 mpaka 4 hadi
8" alisema.
Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka mitatu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment