Saturday, October 20, 2007

LUCKY DUBE SASA YUKO JUU ZAIDI!



kufuatia kifo chake kilichotokea usiku wa kumakia jana, muziki wake hivi sasa uko juu ZAIDI nchini Tanzania, kila kituo cha redio, televisheni, majumbani na maofisini, unapigwa muziki wake na wimbo ambao uko juu kuliko yote, ni ule uitwao REMEMBER ME ambao kwa sasa unaonekana kuendana na tukio la msiba uliowakumba wapenzi wote duniani wa muziki wa reggae na wapenda amani kwa ujumla.

Ni huzuni na ni jambo la kujiuliza, kwa nini maisha ya wanamuziki maarufu wa Reggae duniani huzimika ghafla? Yu wapi Bob Marle, yu wapi Peter Tosh?

WAZIRI MKUU ZIARANI MBEYA

Waziri Mkuu, Edward Lowassa akionyeshwa bonde la Ihefu wilayani Mbarali ni Mkuu wa wilay hiyo, Hawa Ngulume wakati alipotembelea bonde hilo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya.

Waziri Mkuu,Edward Lowassa akizungumza na mmoja wa watoto (jina halikupatikana) waliojitokeza katika mapokezi yake wakati alipowasili katika mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya jana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, October 19, 2007

MOB JUSTICE: NANI WA KULAUMIWA?





Picha zinaonesha tukio la kijana kuchomwa moto juzi asubuhi kwa tuhuma za KUTAKA kuiba kwenye nyumba moja ya mkazi wa eneo la Bonde la Msimbazi jijini Dar es salaam. Vijana hao wanaodhaniwa kuwa vibaka, walikuwa kundi na baada ya kukurupushwa katika jaribio lao la kutaka kuiba, walikimbia lakini kijana pichani alidakwa na wananchi wenye hasira na kupigwa kiberiti LIVE tena mbele ya watoto! JE NANI WA KULAUMIWA, wananchi wenye hasira au vibaka?

NG'OMBE KICHAA!

Mdau mmoja kanitumia hii..!

POLE NAKAAYA!

Mrembo huyu kafanya nini? nenda hapa:WWW.GLOBALPUBLISHERSTZ.COM wamerudi tena FULL!

Wednesday, October 17, 2007

IT'S FUNNY TIME!



Dear Mr. Bill Gates,

This letter is from Masawe of Kibosho Moshi., Tanzania.

We have bought a computer for our home and we found problems, which
I want to bring to your notice.

1. After connecting to Internet we planned to open e-mail account and
whenever we fill the form in Hotmail in the password column, only
****** appears, but in the rest of the fields whatever we typed
appears, but we face this problem only in password field.

We checked
with hardware technician Kimaro and he said that there is no problem in
keyboard.

Because of this we open the e-mail account with password *****. I
request you to check this as we ourselves do not know what the
password is.

2. We are unable to enter anything after we click the "Shut Down"
button.

3. There is a button "Start" but there is no "Stop" button. We request
you to check this.

4. We find there is "Run" in the menu. One of my friend clicked "Run"
has run up to Marangu. So, we request you to change that to
"Sit", so that we can click that by sitting.

5. One doubt is that any "Re-Scooter" available in system? As I find only "Re-Cycle", but I own a scooter at my home.

6. There is "Find" button but it is not working properly. My wife lost
the door key and we tried a lot for tracing the key with this
'Find', but unable to trace. Is it a bug??

7. Every night I am not sleeping as I have to protect my "Mouse" from
CAT, So I suggest you to provide one DOG to kill that cat.

9. My child learnt "Microsoft Word" now he wants to learn "Microsoft
Sentence", so when will U provide that?

Best regards,
Masawe.

LOGO MPYA YA ATCL!




Wandugu, Wajameni,
Nimeongelea mengi katika mazuri yanayofanywa na serikali yetu likiwa pamoja na lile la serikali kuisaidia Air Tanzania. Nilifurahishwa pale CEO huyu mpya, David Mattaka, alipotangaza mipango ya ndege mpya pamoja na uamuzi wake wa kutumia Mercator service kwa ajili ya Revenue accounting.

Nimesikitishwa na yeye kuamua kuitupilia mbali logo yetu ya zamani ya Air Tanzania:
Na kutuletea logo mpya iliyokuwa designed na wakenya ambayo inafanana na ile ya Kenya Airways.

Hivi tumeishiwa creativity kabisa na tumeamua kuwa copycats?
Naomba mchango wenu kabla ya kumuandikia CEO rasmi kumuomba alifikirie hili.

SASA SISI WANANCHI WENYE UCHUNGU NA NCHI HII TUNAOMBA ATAKAYEPOKEA EMAIL HII AIFIKISHE KWA TOP MANAGEMENT.......
Asante Watanzania Masembo K,

warning: USIDANGANYIKE NA EMAIL FEKI KAMA HIZI!

Yahoo Warning!!! Verify Your Account Now To Avoid It Closed ( VX2G99AAJ )...
Standard Header|Full Message View
[Chat now] Yahoo !!
[Chat now] Yahoo !!

Account Alert

VERIFY YOUR FREE YAHOO ACCOUNT NOW !!!

Dear Account User,
This message is from yahoo message center to all yahoo free account owners and premium account owners. We are currently upgrading our data base and e-mail account center. We are deleting all unused yahoo account to create more space for new accounts.

To prevent your account from closing you will have to update it below so that we will know that it's a present used account.

Confirm Your Account Details


Yahoo! ID:........................


Password:........................


Your Birthday:..................

Your Country or Territory:...........

Enter the letter from the Security Image :............ Registration Verification Code

Warning!!! Account owner that refuses to update his or her account before two weeks of receiving this warning will lose his or her account permanently.

BW' MDOGO ALA BINGO ZA TIGO!

Meneja wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya simu ya tiGO, Bw. Kelvin Twissa (kushoto) akimkabidhi shilingi milioni tatu Bw. Salum Adam mara baada ya kushinda Bahati Nasibu ya Matajiri wa tiGO inayoendelea kila wiki.

Mshindi wa kwanza wa Bahati Nasibu hiyo Bw. Salum Adam akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa tatu, Margareth Mandari (kushoto) aliyejishindia sh. 330,000 na mshindi wa nne Fakia Said aliyejishindia 290,000. Washindi hao walikabidhiwa zawadi hizo katika Makao Makuu ya kampuni ya tiGO yaliyopo mtaa wa Lugoda jijini Dar es Salaam .

Bw. Salum Adam (katikati) akihesabiwa pesa zake na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, anaeshuhudia (kulia) ni Afisa wa Value Added Services Technical Assistant wa kampuni hiyo, Bw. Salim Madati

Tuesday, October 16, 2007

YOU ARE WHAT YOU EAT!


VIDONDA VYA TUMBO:

Husababishwa na unavyokula!

Kama tulivyoona wiki iliyopita kwamba staili na aina ya chakula unakachokula ndicho kinachokufanya uwe mnene au mwembemba, leo pia tutaelezea kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, ambao nao unatokana na jinsi unavyokula na unaweza kuudhibiti kwa vyakula tu.

Kitabibu au kitaalamu, vidonda vya tumbo vinaelezewa kama ni ile hali ya kuwepo kwa vidonda kwenye utumbo mrefu au mfupi, kwa ndani. Vidonda vilivyopo kwenye kona ya utumbo mfupi vinajulikana kama Duodenal ulcers na vile vya kwenye utumbo mpana (tumbo) ni Gastric ulcers.

DALILI KWAMBA UNA VIDONDA VYA TUMBO

Dalili kwamba una vidonda vya tumbo ni nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni kusikia maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo kwa wenye vidonda kwenye utumbo mfupi. Maumivu ya vidonda kwenye utumbo mrefu, mara nyingi huja saa moja baada ya mlo na mara chache huja usiku.

Maumivu ya vidonda vya kwenye utumbo mfupi, mara nyingi huja kabla ya mlo, pale tumbo linapokuwa tupu, yaani mtu anaposikia njaa. Maumivu hayo huondolewa kwa chakula, hasa maziwa ambayo yameonekana kuwasaidia watu wengi kupoza maumivu yake.

Vidonda vinapoendelea kuwepo kwa muda mrefu, maumivu huwa makali zaidi na husababisha mwili kudhoofika na kukosa nguvu. Vile vile hali inapoendelea kuwa mbaya zaidi, kinyesi cha mwathirika hutoka na damu.

KITU GANI KINACHANGIA VIDONDA HIVI?

Kitu kinachochangia mtu kupata vidonda vya tumbo ni chakula tu. Aina ya chakula na jinsi unavyokila ndiyo 'mama' wa tatizo hili, matatizo mengine ya kimaisha na msongo wa mawazo au baadhi ya madawa ni miongoni mwa vitu vinavyofanya tatizo kuwa gumu zaidi lakini siyo chanzo. Stali yako ya ulaji inapokuwa nzuri, matatizo mengine hudhibitiwa kwa lishe tu.

Vidonda vya tumbo ni matokeo ya tumbo kuwa na gesi nyingi ambayo husababishwa na ulaji mbovu, kama vile kula na kushiba kupita kiasi, kula vyakula vyenye viungo vingi vikali kama pilipili, unywaji sana wa kahawa, pombe na uvutaji sigara. Ukiwa na staili ya maisha kama hii, lazima utapata vidonda vya tumbo na hakuna dawa ya kuponya ila kufuata kanuni za ulaji sahihi.

Wakati tukikueleza hapa baadhi ya vyakula vitakavyoweza kukupa nafuu ya vidonda, lazima staili yako ya ulaji pia nayo ibadilike.

NDIZI MBIVU KAMA TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

Inaelezwa na wataalamu wetu wa tiba mbadala kuwa ndizi mbivu ni moja kati ya tiba za nyumbani zenye nguvu sana katika kutibu tatizo la vidonda vya tumbo. Tunda hili, ambalo upatikanaji wake hauna shida wala msimu kwa kila mtu, linaaminika kuwa na virutubisho vya ajabu visivyojulikana, ambavyo kiutani wamevipachika jina la Vitamini U (against ulcers)!

Ndizi inapoliwa na ikifika tumboni, ina uwezo wa kutuliza makali ya gesi na kupunguza kuuma kwa vidonda kwa kuuwekea kinga utumbo mzima. Ili upate faida za ndizi kama tiba, hasa kwa wale ambao wako katika hatua za mwanzo za kuumwa vidonda, kula ndizi mbivu mbili pamoja na maziwa mara tatu au nne kwa siku. Fanya hivyo kama sehemu ya mlo wako kila siku.

KABICHI KAMA TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

Kama ilivyo kwa ndizi, kabichi nayo inaaminika kuwa tiba nzuri ya nyumbani ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Chukua robo kilo ya kabichi, ichemshe na maji ya nusu lita hadi yabaki robo. Kisha yachuje na uyaache yapoe. Yakisha poa, kunywa mara mbili kwa siku.

Aidha, mbali ya kuchemsha na kunywa maji ya kabichi, pia unaweza kutengeneza juisi yake ambayo nayo ni bora kwa matatizo ya vidonda vya tumbo. Kwa kuwa juisi ya kabichi ina nguvu sana, itapendeza ikichanganywa na juisi ya karoti kwa kipimo cha nusu kwa nusu na kisha kunywa mara mbili kwa siku.

MAZIWA YA MBUZI KAMA TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.

Mbali ya kula ndizi mbivu pamoja na maziwa ya ng'ombe, kunywa maziwa ya mbuzi peke yake nayo ni dawa kubwa ya vidonda vya tumbo. Ili kupata matokeo mazuri na kwa muda mfupi, kunywa glasi moja ya maziwa ya mbuzi ambayo hayajachanganywa na kitu kingine, mara tatu kwa siku.

MLO WA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

Mlo wa mtu mwenye vidonda vya tumbo unapaswa kupangiliwa kwa makini zaidi ili kutoa lishe inayotakiwa mwilini na wakati huo huo kutoa kinga kwa utumbo ulioathirika na vidonda. Maziwa, krimu, siagi, matunda, mboga mboga, vyakula vingine vya asili vyenye vitamini mbalimbali, ndiyo mlo wa kila siku anaopaswa kula mtu mwenye vidonda.

TIBA NYINGINE

Masaji (massage) ya mwili mzima pamoja na mazoezi ya kuvuta na kutoa pumzi ni miongoni mwa vitu vinavyosaidia kutuliza au kudhibiti vidonda vya tumbo. Mbali na yote hayo, mgonjwa anapaswa kuachana na mawazo na badala yake awe mwenye furaha, hivyo hana budi kutengeneza mazingira ya kuwa mbali na vitu vinavyomkasirisha na kumletea mawazo.

Mufti, Masheikh watimuliwa Ikulu


Elvan Stambuli na Makongoro Oging’ (Gazeti la Uwazi - Okt 16)

Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Simba ambaye alialikwa katika karamu ya Sikukuu ya Idd ya Rais Jakaya Kikwete Ikulu na kumtuma msaidizi wake Naibu Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi akiwa na Masheikh wengine, walijikuta wakitimuliwa Jumamosi iliyopita.

Habari zilizolifikia gazeti hili siku ya tukio zinasema wakati wa kwenda Ikulu jijini Dar es Salaam, Naibu Mufti Sheikh Zuberi alifuatana na viongozi wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) akiwemo Katibu wa Baraza la Ulamaa na Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Sheikh Hassani Chizenga na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Abdallah Nyasi.

Wengine ni Katibu wa Hija, Sheikh Sued Sued, Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje wa BAKWATA, Sheikh Iddi Hussein, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Nguruko na Katibu wake Alhaji Suleiman Magubika.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinasema Masheikh hao walikwenda Ikulu baada ya kualikwa na Rais Kikwete huku Naibu Mufti, Sheikh Zuberi akimuwakilisha Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Simba ambaye alikuwa katika shughuli za sikukuu ya Iddi za kitaifa iliyofanyika mjini Lindi na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein.

Mara baada ya kupata habari hizo waandishi wetu walikwenda Makao Makuu ya BAKWATA na kuwakuta viongozi wote waliotimuliwa Ikulu wakiwa wanatafakari hali hiyo chini ya mwembe ambapo baada ya kuulizwa kuhusu habari hizo walikiri kutokea.

Hata hivyo, Naibu Mufti alimruhusu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ali Nguruko kuzungumza na Uwazi ambapo alisema wamefedheheshwa sana na waliyofanyiwa Ikulu.

Akifafanua zaidi Sheikh Nguruko alisema Rais Kikwete aliswali swala ya Iddi katika Msikiti wa Al Farouk, Makao Makuu ya BAKWATA na akaagiza Naibu Mufti na viongozi wenzake waende Ikulu katika karamu aliyoiandaa bila kukosa.

"Rais Kikwete aliagiza kuwa Naibu Mufti na jopo lake waende Ikulu kwa sababu ameandaa karamu, tuliondoka baada ya kuagana na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye pia aliswali hapa, tulipofika getini Ikulu tulipekuliwa kwa kufunuliwa kanzu zetu, hata Naibu Mufti alifunuliwa, tulisikitika sana, tulijiuliza hawa hawajui kuwa Masheikh hawa ndio waliomswalisha Rais leo," alisema Sheikh Nguruko.

Aliongeza kuwa kilichowasikitisha zaidi ni kuona raia wa kigeni wakipita na kuingia Ikulu bila kupekuliwa kama alivyofanyiwa Naibu Mufti na wao lakini kibaya zaidi alisema ni kitendo cha jopo zima la Bakwata kutoruhusiwa kuingia Ikulu kama alivyoagiza Rais Kikwete.

"Kwanza wale watu tuliowakuta getini walipaswa kujua kwamba Naibu Mufti ana heshima yake kitaifa na pia alikuwa akimuwakilisha Mufti wa Tanzania, sasa kumpekua mpaka kwenye mkanda na kumkatalia kuingia tumeona kuwa wamemdharau na kumdhalilisha kiongozi wetu, "alisema Sheikh Nguruko.

Naye Katibu wa Ulamaa, Sheikh Chizenga alisema kwamba hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wakuu wa BAKWATA kukataliwa kuingia Ikulu katika sherehe ya Iddi kwani viongozi wa awamu zote tatu za serikali zilizopita walikuwa hawafanyi hivyo, hivyo kuwatupia lawama watendaji wa Ikulu na sio Rais Kikwete.

"Kiongozi Mkuu wa nchi kama Rais Kiwete anapotoa agizo watendaji ni lazima watekeleze, hatukuona sababu ya kutoruhusu msafara wa Naibu Mufti kukwama kuingia Ikulu kwani licha ya kumwakilisha Mufti Mkuu Tanzania, Rais Kikwete alitoa mwaliko hadharani na kusisitiza kwamba shughuli yake itachelewa kuanza kutusubiri sisi, tukakwama getini," alisema Sheikh Chizenga.

Alibainisha kuwa walijaribu kuwasihi maofisa waliokuwa getini wawaruhusu kuingia lakini walikataa kata kata na kwamba japokuwa yeye (Sheikh Chizenga) aliruhusiwa kuingia hakukubali kufanya hivyo kwa kuwa Naibu Mufti alikataliwa hivyo naye kususa kuingia kwenda kwenye shughuli hiyo ya Rais Kikwete.

Aidha Sheikh mwingine aliyesusa kuingia Ikulu ni Sheikh Yahya Hussein ambaye alipofika getini aliruhusiwa lakini mtoto wake wa miaka mitano alizuiliwa na akaambiwa yeye aende lakini mtoto abaki getini.

"Nilisema haya mambo ni ya ajabu, nitamuachaje mtoto getini? Walikataa kumruhusu mtoto basi tukakusanyana na masheikh wengine tukajiondokea na kuja nyumbani kwangu kunywa chai,'' alisema Yahya.

J.K ULAYA TENA

Rais Jakaya Kikwete akizunumza na Makamu wa Rais, Dr. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu,Edward Lowassa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka kwenda Italia na Ufaransa jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

YANGA KWA WAKA MOTO BAADA YA MFADHILI MANJI KUTANGAZA KUJITOA, MADEGA KUSHIKA HATAMU NA KUMPONDA!

SISI NDO YANGA..NA TANGA NDO SISII, ALAAA!!!!
tunasema hatumtaki Manji
We unakubalina na hoja ya Madega kwelii?
Yanga klabuni..a.k.a Mtaa wa jangwanii..
Mi ndo Yusuf Mzimba.. Yanga asili haswaa..
..askari wale kulee..
Mtuelewe, sisi ndo wazee wa yanga..
tusikilizane, Madega hatufaii...
hapiti mtu hapa, ala!

Monday, October 15, 2007

KUMEKUCHA BONGO STAR SEARCH 2008!

Kumekucha Bongo Star Search 2007/8..msululu wa vijana wakijaribu bahati zao Leaders club Jumamosi
Salama Jabir..jaji machachari wa shindano
Rita Paulsen..mwanzilishi bongo Star Search na jaji pia...
Master Jay...producer wa muziki na jaji pia wa Bongo Star search
Majaji kazini
chukua namba yako..

Washindi 15 BSS Dar kupatikana leo

Baada ya kuzunguka kunako mikoa mitano ya Tanzania Bara na visiwani, hatimaye mpambano wa kumsaka Staa wa Bongo unaojulikana kama Bongo Star Search umevamia Dar es Salaam kwa mafanikio ya kutosha ambapo washindi 15 watapatikana leo katika Viwanja vya Leaders Club, inashushwa na Julius Kihampa.

Fainali hiyo kubwa ilianza kuunguruma Jumamosi ya wiki iliyopita, ambapo 15 watakaopatikana leo watajiunga na wale 25 waliopatikana katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Zanzibar na kuingia katika hatua nyingine ya mchujo.

Wakati mpambano huo unaanza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, zaidi ya vijana 1000 walijitokeza kushiriki na kusababisha foleni ambayo haielezeki, katika zoezi hilo wengine walipatikana jana.

Aidha mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo, Rita Paulsen, alisema kuwa amefarijika kuona vijana wengi waliojitokeza na amewataka wote wanaotarajia kuchujwa leo kuonesha uwezo wao bila woga.

Nature ala shavu Big Brother


Baada ya kuibuka na tunzo ya Channel O, kupitia video yake ya Mugambo kwenye sherehe zilizofanyika Johannesburg, Afrika Kusini wiki iliyopita, msanii Juma Kassim Kiroboto Nature amekula shavu la kupiga shoo katika fainali kubwa za shindano la Big Brother Afrika linaloendelea nchini humo.

Akiongea na Abby Cool & MC George Over The Weekend muda mchachae baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere, huku akiwa na tunzo hiyo mkononi, Nature alisema kwamba mbali kufanikiwa kuibuka na ushindi huo pia amepata dili ya kwenda kupiga shoo siku ya fainali ya shindano la Big Brother itakayofanyika siku chache zijazo.

'Natarajia kwenda tena Afrika Kusini Novemba 4 kwa ajili ya shoo moja ya Big Brother, nawashukuru sana Watanzania na wote walionipigia kura mpaka kufanikiwa kuleta heshima nyumbani' alisema msanii huyo ambaye katika tuzo hiyo aliwamwaga wasanii kibao kutoka Afrika Mashariki.