Thursday, January 17, 2008

KANUMBA NDANI YA V.O.A!


Kanumba akihojiwa na mtanazaji wa kituo cha redio cha Voice of America (VOA) na kipindi chake kitarushwa hewani Jumapili ya tarehe 27 mwezi huu jioni saa moja na nusu, kwa wabongo wanaweza kunasa kupindi hicho Radio Tumaini au Radio Free Africa........kazi kwenu!

2 comments:

Anonymous said...

Even I can get some airtime on VOA,step your game up!

Anonymous said...

Anonymous wa kwanza unajua kabla ya kumcriticize Kanumba inapaswa ujua hali ya wacheza film Tanzania.

1. Wengi wanaganga njaa na kutafuta umaarufu wa bure.

2. Wanalipwa pesa mbuzi sana. Si ajabu kukuta mtu anacheza scene 9 au kumi analipwa Tshs. 30,000/ kwa scene zote. Pia wako wengi tu wanaocheza bure ili waonekani tu kwenye TV.

3. Juzi nimepata dondoo moja ya ajabu. Tanzania House of Talent waliitisha wasanii kuja kushoot tamthilia eti waigize tamthilia yenye urefu wa episode ngapi sijui kwa dau la Tshs. 5,000/- (elfu tano tu) kwa kila msanii.

Kwa hiyo mnapomjaji Kanumba mjue kuwa ametoka katika background hiyo.

Hii safari aliyodhaminiwa kanumba kwenda kutalii Marekani imeacha gumzo si kitoto katika jamii ya waigizaji wengine aliowaacha hapa Bongo. Yaani kwa ufupi kwa mazingira yao Kanumba ameukata na anakula kuku.

Hizo picha za tuzo feki alizopiga akirui katika circle yake ya wasanii atatamba si mchezo.

Na tatizo ni kwamba wengi wataamini kuwa amepata tuzo huko Marekani.

Na tatizo zaidi wale watakaoamini hawatakuwa tayari kusikiza criticism toka kwa wajuaji wa mambo kama kina sisi kwa kuwa tunaonekana kama tunabeza juhudi za wasanii wa filamu Bongo.

Naomba kuwakilisha.