Monday, August 27, 2007

MEDDY MPAKA NJIA!


Na Waandishi Wetu

Uvumi kuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Mpakanjia amefariki dunia, umezua vilio kila kona ya nchi huku baadhi ya ndugu na marafiki zake wakikusanyika nyumbani kwake wakidhani kuna msiba.

Vilio hivyo, vilitawala sambamba na ndugu pamoja na marafiki wa Mpakanjia kumiminika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo, Jumamosi iliyopita, baada ya uzushi kuzagaa kuwa amefariki dunia.

Ndugu mmoja wa Mpakanjia ambaye aliomba hifadhi ya jina lake gazetini, aliliambia Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu juzi kuwa, familia ya mfanyabiashara huyo imehuzunishwa na habari hizo za uzushi.

“Hapa tupo nyumbani kwa Medi (Mpakanjia), baadhi ya watu wamekusanyika wanadhani kuna msiba, wanalia sana, hawatuamini tukiwaambia kuwa Medi hajafa, isipokuwa ni kweli anaumwa.

“Kimsingi kuna watu wabaya wanamchuria ndugu yetu, hatujui watapata maslahi gani Medi akifa,” alisema ndugu huyo kwa uchungu.

Aidha, ndugu huyo alisema, uzushi wa namna hiyo ulijitokeza hata kwa aliyekuwa mke wa Mpakanjia, Marehemu Amina Chifupa kabla hajafa, kwani baadhi ya watu walianza kumchuria kifo mapema.

Kufuatia habari hizo za Mpakanjia kufa, watu mbalimbali walilipigia simu gazeti hili, wengine wakilitumia ujumbe mfupi wa maneno (sms), wakitaka kupata uhakika huku baadhi yao wakitoa salamu za rambirambi.

Simu na sms hizo zilimiminika kwenye ofisi ya gazeti hili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, kudhihirisha namna uvumi huo ulivyopata umaarufu katika kona mbalimbali za nchi.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu wikiendi iliyopita umebaini kuwa, Mpakanjia bado yupo hai, ingawa hali yake ni mbaya na amelazwa kwenye Hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba, mfanyabiasha huyo amelazwa kwenye wadi ya watu maalumu (VIP), lakini anakula na kujisadia haja ndogo kwa msaada wa mipira.

Ijumaa Wikienda linatoa pole kwa familia ya Mohammed Mpanjia kuhusiana na uvumi wa habari hizo za kifo, pia linamuombea afya njema mfanyabiashara huyo ili arejee katika hali nzuri.


BUBU HUYU HAFAI...

Inatoka Uk 1
Bubu huyo ambaye ni mkazi wa Iringa mjini, anamiliki danguro hilo ndani ya moja ya gesti zilizopo kwenye Eneo la Mshindo, mkoani humo.

Vyanzo mbalimbali vya gazeti hili, vilieleza kuwa mbali na kufanya biashara hiyo, pia Shambe huwapigisha picha za utupu warembo anaowamiliki na kuziuza kama mali halali.

Vyanzo hivyo viliongeza kuwa mlemavu huyo huwauza mabinti wa danguro lake kwa gharama tofauti, kulingana na muda ambao mteja atahudumiwa, pia thamani ya picha huendana na ubora pamoja na uzuri wa wapigwaji.

“Kwa mfano, mteja akitaka kulala na mwanamke mmoja kuanzia usiku hadi asubuhi, Bubu huwa anawatoza shilingi 2,500 hadi 3,000, lakini kama atataka huduma ya ‘chapu chapu’ huwa wanamlipa shilingi 1,000 au 1,500,” kilisema moja ya vyanzo vyetu.

Ilielezwa na chanzo kingine kuwa Shambe ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Bubu, mara nyingi huzingatia uzuri na umri wa binti anayemmliki.

“Wale ambao ni wazoefu gharama yake siyo kubwa, lakini mabinti wadogo na wanawake wenye mvuto, mara nyingi bei zao hufikia mpaka shilingi 5,000.

“Hata kwenye picha, kama picha ni nzuri na wanawake ni warembo huziuza kwa shilingi 2,000, kama ubora wake ni mdogo huziuza kwa shilingi 1,500 au 1,000,” kilisema chanzo chetu kingine.

Wiki iliyopita, gazeti hili, lilimtuma mwandishi wetu, Iringa, kwenda kufanya upelelezi kwenye gesti inayodaiwa kutumiwa na Shambe kama danguro.

Katika upelelezi huo, mwandishi wetu alifanikiwa kumpata Shambe ambapo alimlipa shilingi 1,000 na kukabidhiwa mrembo mmoja katika kipindi cha saa mbili.

Aidha, mlemavu huyo alimuuzia mwandishi wetu picha tofauti za utupu ambazo aliwapiga mabinti waliopo kwenye danguro lake na nyingine akiwa amepozi nao.

Katika mahojiano na mwandishi wetu, dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Anitha ambaye ni mmoja wa mabinti waliopo kwenye danguro la Shambe, alisema, wanalazika kufanya kazi hiyo kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Anitha aliongeza, yeye kama walivyo wenzake wametokea kwenye vijiji tofauti mkoani Iringa na waliangukia kwenye danguro la Bubu baada ya kukosa uelekeo wa kimaisha mjini.

Alisema, licha ya kwamba Bubu huwa anawalipa vizuri lakini hapendi kujiuza kwakuwa ni hali ya kujidhalilisha.

Ijumaa Wikienda bado lipo kwenye mapambano ya vitendo hatarishi vya gonjwa hatari la ukimwi, hatupendi ndiyo maana tunayaweka wazi kwa jamii ili wanaohusika wafuatilie na adhabu kali ichukuliwe kwa waharibifu.
Mhariri.
(pichazaidi: http://www.globalpublisherstz.com/2007/08/26/meddy_mpakanjia.html)

No comments: