Monday, August 27, 2007

WASANII WA BONGO FLAVA NA TAIFA STARS!

Hivi sasa karibu kila kona ya Bongo, gumzo kubwa ni mechi kati ya timu yetu ya Taifa na Msumbuji ambayo inatarajiwa kupigwa Septemba 8, mwaka huu ndani ya uwanja mpya wa Taifa, sisi kama Abby Cool & MC George Over The Weekend, kupitia kitengo hiki cha ÔStreet VersionÕ hatupo nyuma katika kuonesha uzalendo.

Wanaharakati ya safu hii waliingia mtaani ili na kupiga stori na watu wawili watatu ambao majina yao yanajulikana kwa sana katika jamii yetu. Kikubwa ilichokuwa inataka iwaletee wasomaji ni kauli za mastaa hao ambao kwa nyakati tofauti waliulizwa kwamba ÔWewe kama Mtanzania una maoni gani kuhusu mechi kati ya Stars na Msumbiji?. Haya ndiyo maoni yao:

Jina:Khadija Shabani (K-Sher- (PICHANI JUU)
Maoni: Japo siko karibu sana na mambo ya michezo, napenda kuwaambia Watanzania wenzangu kwamba, sisi kama wazawa tuwe kitu kimoja katika kushangilia na kuhakikisha Stars inafanikiwa kuishinda Msumbiji na kuendelea na michezo mingine huko mbele.
Kwa sababu ushindi huo ni sifa kwa taifa zima, siyo mtu mmoja. Niko pamoja na timu yetu
Jina: Said Fella (Mkubwa)
Maoni: Nikiwa kama Mtanzania, wananchi tuwe wamoja, tuombe Mungu apokee dua zetu ili vijana waende Ghana, kwani kwenda huko ni kufungua soko jipya la mpira na kumuenzi Rais mstaafu, Mkapa na uwanja wetu mpya, kumpa moyo Rais Kikwete kwa kuwapa moyo wachezaji mpaka hapo walipo sasa. Vilevile wachezaji wakaze buti, wasituangushe kwani wakicheza vizuri ni maisha mazuri kwao na taifa kulitangaza na kushangilia.

Jina: Abdul Sykes (Dully Sykes)
Maoni: Mi sina cha zaidi cha kuongelea, ila timu yetu naiamini, nategemea ushindi na si kitu kingine.

Jina: Gervas Kasiga (Chuma)
Maoni: Kikubwa Watanzania wote kuwa na uzalendo kwenye mechi hii, tufute itikadi zetu za kisiasa, kiimani na kitimu. Ushindi kwetu uwe ni wa lazima ili walau tuweze kujiliwaza na ugumu wa maisha unaotuandama, tukumbuke ushindi wa Stars kwa namna moja utakuwa umeongeza nafasi za ajira kwa Watanzania wengi, hususasi wale wote wajasiriamali watakaojiusisha na mauzo ya jezi za Stars, bahati nasibu, documentary, naimani kubwa na wachezaji kwa sababu serikali imeshawajenga, hivyo Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya wao tayari wanayo. Tunachohitaji kwao ni ushindi.

Jina: Selemani Msindi Afande Sele (PICHANI JUU)
Maoni: Mimi naamini timu iko bomba kutokana na mabadiliko makubwa wanayoonesha uwanjani, ukilinganisha na zamani, halafu uzalendo wa Rais JK katika timu pia ni nusu ya kushinda. Ila kocha bado anaweza kuongeza wachezaji kama Machupa, Pawasa, Mrisho Ngasa kuipa nguvu ya ushindi wa uhakika kwa kuzingatia matokeo mabovu tuliyoyapata katika ziara ya Denmark ingawa tunacheza na timu za kawaida kama vile Ghana walivyocheza na Brazil. Watu wanahitaji furaha kupitia kwa timu hiyo, kocha asipuuze mawazo ya wataalam wetu, wazalendo na makocha wa zamani

No comments: